Sheria na Kuzuia Uhalifu

Wajumbe wa Kundi la Kazi la UM kwa waliopotezwa na kutoweka wahitimisha kikao cha 88 Rabat

Wajumbe wa Kundi la Kufanya Kazi la UM juu ya Watu Waliolazimishwa Kupotea na Kutoweka baada ya kukukamilisha ziara yao ya siku nne katika Morocco walikutana kwenye mji wa Rabat na kukamilisha kikao cha 88 kilichofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Juni walipozingatia masuala yanayohusika na watu kukamatwa kimabavu na kutoweka wasijulikane walipo.

KM amehuzunishwa sana na uvamizi wa kunajisi kimabavu wanawake wafungwa katika JKK

KM Ban Ki-moon ametangaza kuhuzunishwa sana na ripoti alizopokea karibuni, kuhusu tukio la uvamizi na vitendo vya kunajisi kimabavu, wafungwa wanawake 20 waliojaribu majuzi kukimbia kutoka gereza kuu la Goma, liliopo katika eneo la mashariki ndani ya JKK.

Idadi kubwa ya wakazi wa eneo la mapigano katika JAK wamehajiri mastakimu: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mashambulio yaliotukia Ijumapili alfajiri, tarehe 21 Juni, kwenye mji wa Birao, kaskazini-mashariki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yamesababisha idadi kubwa ya wakaazi kuhama kidharura eneo hilo.

Idadi kubwa ya wahamaji wa Usomali na Ethopia wanaotoroshwa Afrika Kusini huteswa na wafanya magendo, inaripoti IOM

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limetoa ripoti mpya kuhusu "uhamaji usio wa kawaida" ambao huwatesa wale watu wanaotoroshwa kimagendo kutoka Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, wanaopelekwa Afrika Kusini.

ICTR imetangaza kifungo cha miaka 30 kwa mtuhumiwa Kalimanzira

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imetangaza hukumu ya kifungo cha miaka 30, kwa Callixte Kalimanzira, aliyekuwa ofisa Mkurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Rwanda katika 1994, ambaye alipatikana na hatia ya jinai ya mauaji ya kuangamiza makabila, na pia makosa ya kuchochea watu kuendeleza mauaji ya halaiki.

ICC yathibitisha kesi kwa aliyekuwa naibu-raisi wa JKK

Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) imethibitisha kuwa kuna ushahidi wa kuridhisha wa kuanzisha kesi ya kumtuhumu Jean-Pierre Bemba Gombo, aliyekuwa naibu-raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), kwamba alishiriki kwenye makosa ya vita na jinai iliotengua haki za kiutu.

Mapigano Usomali yazusha msururu was maafa, mamia ya majeruhi na uhamisho wa lazima

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mapigano makali yalioshtadi katika mji mkuu wa Mogadishu, Usomali mnamo miezi ya karibuni, yamewacha nyuma msururu wa uharibifu na maangamizi, majeruhi kadha wa kiraia na kusababisha mamia elfu ya watu kulazimika kuhama makazi na kuelekea maeneo tofauti ya nchi yenye hifadhi bora.

Hali ya usalama wa kigeugeu Kivu Kaskazini inaitia wasiwasi OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali ya usalama wa raia, ulioregarega Kivu Kaskazini, inaitia wasiwasi mkubwa wahudumia misaada ya kiutu waliopo katika JKK.

Uhamisho wa raia Usomali unaendelea kukithiri wakati mapigano yakishtadi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti idadi ya raia waliolazimika kuyahama makazi katika mji wa Mogadishu, tangu mapigano kuanza mnamo tarehe 08 Machi (2009), imekiuka watu 96,000 kwa sasa.

UN-HABITAT/UNIFEM yatashirikiana kupiga vita udhalilishaji na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake

Mashirika mawili ya UM, yaani lile shirika juu ya makazi, UN-HABITAT, na lile shirika linalohusika na mfuko wa maendeleo kwa wanawake, UNIFEM, yameshirikiana rasmi kujumuika bia kukabiliana na tatizo la udhalilishaji na matumizi ya mabavu dhidi ya wanawake na watoto wa kike, katika miji ya mataifa yanayoendelea.