Sheria na Kuzuia Uhalifu

Tume ya UM inajiandaa kuchunguza kesi 500 za watu waliotoroshwa kimabavu

Tume ya Utendaji ya UM kuhusu Watu Waliotoroshwa na Kupotezwa Kimabavu inajitayarisha kufanya mapitio ya kesi 500 ziada za waathiriwa waliotoweka kufuatia ripoti ilizopokea kutoka nchi wanachama 34.

Mataifa Wanachama 125 yanakutana Rio kusailia hifadhi ya watoto na vijana dhidi ya ukandamizaaji wa kijinsiya

Wajumbe karibu 3,000 kutoka nchi 125, wamekusanyika hii leo kwenye mji wa Rio de Janeiro, Brazil kuhudhuria kikao cha siku nne cha Mkutano Mkuu wa Tatu kukomesha dhidi ya Ukandamizaji wa Kijinsiya dhidi ya Watoto na Vijana Ulimwenguni.

Mkataba wa kupiga marufuku mabomu yaliotegwa ardhini unafanyiwa mapitio Geneva

Mjini Geneva, Uswiss kulifunguliwa rasmi, leo hii, kikao cha 9 cha Mataifa Yalioidhinisha Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu Yaliotegwa Ardhini ambapo risala ya Raisi wa mkutano, Balozi Jurg Streuli ilikumbusha kwamba licha ya kuwa mabomu milioni 40 ya kutega yalifanikiwa kuangamizwa kimataifa, mapaka sasa, na wakati huo huo kilomita kadhaa za ardhi zilifufuliwa baada ya mabomu hayo kuteketezwa, hata hivyo majukumu makubwa na mazito bado yamesalia na yatakikana kufyeka silaha hizi ovu katika maeneo kadha wa kadha ya dunia.

UM wahadharisha, watoto mazeruzeru wa Maziwa Makuu wanahitajia hafadhi ya dharura

Mnamo wiki za karibuni, tulipokea taarifa zilizosema binti mmoja zeruzeru, wa umri wa miaka 6, aliuawa katika jimbo la mashariki la Ruyigi, nchini Burundi, ambalo hupakana na Tanzania. Baada ya kuuliwa alikatwa viungo, ktokana na itikadi ya wenyeji, isio sawa, inayoamini viungo hivyo humpatia mwanadamu miujiza na nguvu za kichawi.

UM imewateua majaji watano kutumikia Mahakama ya ICJ

Kuhusu habari nyengine, Baraza Kuu la UM na Baraza la Usalama Alkhamisi limeteua mahakimu watano watakaotumikia Mahakama Kuu ya Kimataifa (ICJ) kwa muda wa miaka tisa, kuanzia mwaka 2009.

Tani 100 ziada za pembe zimeuzwa chini ya uangalizi wa CITES

Taasisi ya CITES, ambayo inahusika na utekelezaji wa Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Aina ya Wanyama na Mimea Pori Adimu imeripoti dola milioni 15 zilifanikiwa kuchangishwa baada tani 102 za pembe za ndovu kuuzwa wiki iliopita, fedha ambazo zitasaidia kutunza bora tembo wa Afrika.