Sheria na Kuzuia Uhalifu

UM inawakumbuka waliopotea kimabavu duniani

Tume ya Utendaji ya UM juu ya Watu Waliotoweka Kimabavu itaadhimisha miaka 25 ya Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Waliotoweka Duniani. Siku hiyo huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 30 Agosti.

Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu za Ukomeshaji wa Biashara ya Utumwa Duniani

Tarehe 23 Agosti inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa juu ya Kumbukumbu za Ukomeshaji wa Biashara ya Utumwa Duniani. ~~~

UNAMIL imeripoti tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia zimepungua Liberia

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Liberia (UNMIL) limewasilisha ripoti mpya kuhusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia nchini, yanayoambatana na watumishi wa UM. Kwa mujibu wa ripoti, idadi ya shutuma za makosa hayo dhidi ya wafanyakazi wa UNMIL imeteremka katika 2008.

UNODC imepongeza kukamatwa afyuni UAE iliovunja rikodi

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Uhalifu na Madawa ya Kulevya (UNODC) imeripoti katika wiki iliopita polisi wa Umoja wa Imarati za Kiarabu (UAE) waliwashika katika Imarati ya Sharjah watuhumiwa 19 wa KiAfghani na kilo 202 za unga wa afyuni iliotakaswa.

Mapinduzi ya karibuni Mauritania yamelaaniwa na BU

Kwenye taarifa iliotolewa na Baraza la Usalama (BU) kufuatia mkutano wa hadhara Ijumanne kuzingatia hali Mauritania, wajumbe wa Baraza walishtumu vikali mapinduzi yaliofanyika na wanajeshi dhidi ya Serikali katika wiki za karibuni.

Wanaotengua haki za ilimu wapewe adhabu, anasihi Villalobos

Vernor Munoz Villalobos, Mkariri Maalumu wa UM juu ya Haki za Kupata Ilimu ametoa taarifa maalumu Geneva inayopendekeza wale wanaoshambulia walimu, wanafunzi na maskuli wakamatwe na wapelekwe mahakamani kukabili haki na kuhukumiwa adhabu kali.

Aliyeokoka shambulio la ugaidi Kenya 1998 kuiomba UM kusaidia kudhibiti tukio kama hilo kimataifa

Mnamo tarehe 07 Agosti 1998 katika mataifa ya Kenya na Tanzania kulitukia mashambulio ya kigaidi yaliosababisha vifo na majeruhi kadha kwa raia wa mataifa hayo ya Afrika Mashariki. Caroline Wavai wa kutoka Kenya ni mmoja wa waathiriwa aliyenusurika na tukio hilo. Baada ya hapo alihamasishwa kuanzisha shirika lisio la kiserekali, linaloitwa Baraka Care International kwa madhumuni ya kusaidia umma kupata kinga bora dhidi ya matukio kama hayo.~~