Sheria na Kuzuia Uhalifu

Ufyekaji wa madawa ya kulevya ni jukumu la wote, anasihi Ban

Tarehe 26 Juni huadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa dhidi ya Matumizi na Biashara Haramu ya Madawa ya Kulevya Duniani.

Mwendesha Mashtaka wa ICC anasihi Lubanga asiachiwe

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) ametoa mwito maakumu unaowanasihi majaji wa korti hiyo kutomwachia mtuhumiwa wa kwanza wa mahakama, Thomas Lubanga aliyekuwa kiongozi wa majeshi ya mgambo katika JKK (DRC). Majaji wa Mahakama ya ICC wanazingatia kumwachia Lubanga kwa sababu ushahidi uliowakilishwa kwenye kesi yake ulikuwa na kasoro kisheria, dhidi yake. Miongoni mwa mashtaka aliotuhumiwa Lubanga ni lile kosa la kuwashirikisha watoto chini ya umri wa miaka 15 kwenye shughuli za vita na mapigano, katika eneo la mamshariki la Ituri, katika JKK. Mtuhumiwa amekataa makosa.~

BU yahimiza hatua kali dhidi ya mateso ya kijinsiya, hasa karaha ya kunajisi kimabavu

Baraza la Usalama limeamrisha kusitishwe, halan, na kwa ukamilifu pote ulimwenguni vitendo vya mateso ya kijinsia dhidi ya raia, ambavyo huendelezwa zaidi kwenye mazingira ya vita na mapigano na makundi yanayoshiriki kwenye vita na mapigano.

UNICEF kushtushwa na kukithiri kwa utekaji nyara wa watoto ulimwenguni

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kushtushwa na muongezeko wa utekaji nyara na utoroshaji wa watoto wadogo vinavyofanywa na maharamia na wahalifu, hasa katika mataifa yaliopambwa na vurugu. Mara nyingi wakosaji hawa huendeleza jinai yao bila adhabu.

WFP yaihimiza jamii ya kimataifa kufadhilia manowari dhidi ya uharamia Usomali

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa ombi maalumu Alkhamisi linayoyataka yale mataifa yenye kumiliki majeshi makuu ya majini, kuisaidia UM kwa kuipatia manowari zao ili kulinda meli zinazochukua shehena ya chakula inayopelekwa Usomali, bidhaa ambayo inatakikana kukidhi mahitaji ya dharura kwa watu muhitaji milioni 2 watahatarishwa na tatizo maututi la njaa na utapia mlo pita watanyimwa posho hiyo.

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki Rwanda kukana makosa

Dominuque Ntawukuriryayo, aliyekuwa ofisa wa Serikali Rwanda na aliyetuhumiwa na Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) kuwa miongoni mwa wachochezi wa mauaji ya halaiki ya raia 25,000 wenye asili ya KiTutsi katika 1994, ameripotiwa kukana makosa mbele ya ICTR mjini Arusha, Tanzania.

ICC inaishtumu Sudan kwa makosa ya jinai Darfur

Baraza la Usalama limekutana kwenye kikao cha hadhara kuzingatia suala la Darfur. Luis-Moreno Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa Juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) alitarajiwa kuwakilisha ripoti maalumu yenye tuhuma zinazolenga wenye madaraka Sudan dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu katika Darfur.

UM imeshtumu mauaji ya ukabila ya raia wa Nigeria katika Ukraine

Jennifer Pagonis, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumanne aliripoti kwa waandishi habari mjini Geneva kuwa wamepokea taarifa zenye kuelezea mauaji ya raia mmoja wa Nigeria katika mji wa Kyiv, Ukraine, mnamo tarehe 29 Mei, mauaji ambayo UNHCR inaamini yalikuwa ya kikabila:~

Baraza Kuu linajadilia biashara haramu ya kutorosha watu

Baraza Kuu la UM Ijumanne lilifanyisha kikao maalumu kujadilia tatizo la kudhibiti biashara haramu ya kuvusha watu, kwa ajira isiokubalika kisheria, ambayo sasa hivi inaendelezwa na kupaliliwa kimataifa.