Sheria na Kuzuia Uhalifu

Ripoti ya UNODC yathibitisha mauaji yamekithiri Kusini ya Afrika na Amerika za Kati na Kusini

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) imechapisha ripoti mpya kuhusu viwango vya mauaji ulimwenguni.

Ofisa mkaazi wa WHO anasema "hali ni ngumu tangu mashambulio kuanzishwa Ghaza"

Leo asubuhi tulipata taarifa ziada kutoka Mahmoud Daher, Ofisa wa Afya anayewakilisha Shirika la Afya Duniani (WHO) katika Ghaza, ambaye alihojiana, kwa kutumia njia ya simu, na Samir Imtair Aldarabi, mwanahabari wa Idhaa ya Kiarabu ya Redio ya UM. Daher alielezea hali ilivyo sasa hivi katika Ghaza, kama ifuatavyo:~

'Utambuzi wa mfumo wa ujinsiya utegemee sera za kitaifa na usishurutishwe kimataifa', nchi wanachama zakumbushana

Kwenye majadiliano yaliofanyika Alkhamisi katika ukumbi wa Halmashauri ya Baraza Kuu juu ya Uchumi na Jamii (ECOSOC) kuzingatia “haki za binadamu, utambulishi wa kijinsiya na ujinsiya”, kulipigwa kura, isiyokuwa na masharti ya kiseheria, ambapo Mataifa Wanachama 66 yalitoa mwito wa kutaka kufutwa kwenye sheria zile amri zinazotafsiri vitendo vya ubasha, usagaji na usenge kuwa ni uhalifu. Kikao hiki kilidhaminiwa na balozi za mataifa ya Argentina, Brazil, Croatia, Gabon na pia Norway, Ufaransa na Uholanzi

Wanajeshi wa zamani watatu wa Rwanda wahukumiwa kifungo cha maisha na ICTR

Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) Alkhamisi imetoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa maofisa watatu, wa vyeo vya juu, wa jeshi la Rwanda la 1994.

Walimwengu wanaadhimisha Siku ya Kimataifa Kupiga Vita Ulaji Rushwa.

Tarehe ya leo, Disemba 09, inaadhimishwa ulimwenguni kuwa ni Siku ya Kimataifa Kupiga Vita Ulaji Rushwa. Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Uhalifu na Madawa ya Kulevya (UNODC) imeanzisha, kwenye siku hii, kampeni ya kuhimiza umma wa ulimwengu, katika sehemu zote za dunia, kuwa na msimamo imara dhidi ya matatizo ya ulaji rushwa kwenye maeneo yao.

Darzeni za mataifa yamechangia kutia sahihi Oslo mkataba wa kupiga marufuku mabomu ya mtawanyo

Kuanzia tarehe 02 mpaka 04 Disemba, wawakilishi wa kutoka nchi 100 ziada walikusanyika kwenye mji wa Oslo, Norway kutia sahihi mkataba uliodhaminiwa na UM, wenye kuzitaka nchi wanachama zote kuahidi kuwacha kutengeneza, kutumia au kurimbikiza na kuhamisha zile silaha za mabomu ya mtawanyo, yaani zile silaha ambazo mara nyingi huua raia wasio hatia, na kulemaza jamii mbalimbali za umma wa kimataifa, muda mrefu baada ya uhasama kusitishwa. ~~

Tume ya Utendaji dhidi ya Vitendo vya Kutorosha na Kupoteza Watu yakamilisha kikao cha 86 Geneva

Wajumbe wa Kundi la Utendaji la UM kuhusu Masuala ya Watu Wanaotoroshwa na Kupotea wamekamilisha kikao chao cha 86 – kilichofanyika mjini Geneva kuanzia tarehe 26 Novemba hadi Disemba 04, 2008 – kwenye Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu.

Baraza Kuu limepitisha vifungu 57 kuhusu udhibiti bora wa upunguzaji silaha duniani

Kwenye majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu yaliofanyika Ijumanne, hapa Makao Makuu, wajumbe wa kimataifa waliokusanyika kwenye kikao cha wawakilishi wote, walipitisha vifungu 57 vya maazimio, yaliojumlisha, vile vile, maazimio mapya mawili yanayohusu silaha za kawaida, kwa kufuatana na mapendekezo ya Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu, Kamati ambayo huzingatia masuala ya usalama wa kimataifa na shughuli za kupunguza silaha duniani.

Mwendesha Mashitaka wa ICC atoa maelezo maalumu juu ya Darfur kwenye BU

Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki ya ICC, Luis Moreno-Ocampo amewasilisha kwenye Baraza la Usalama (BU) ripoti ya uchunguzi wa Mahakama juu ya madai ya kuendelezwa vitendo vya uhalifu katika Darfur. ~

Kwenye taadhima za Siku ya Kuondosha Utumwa Duniani KM Ban ahadharisha athari za utumwa mamboleo

Mataifa Wanachama wa UM wanaadhimisha Disemba pili kuwa ni Siku Kuu ya Kuondosha Utumwa Duniani.