Sheria na Kuzuia Uhalifu

Vikwazo vya almasi Liberia kuondoshwa na Baraza la Usalama

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Liberia, Alan Doss amepongeza uamuzi wa karibuni wa Baraza la Usalama, wa kuondoa vikwazo dhidi ya biashara ya kuuza almasi kutoka taifa hili la Afrika Magharibi.

UNMIS kulaani mauaji ya ofisa wa jeshi la AU Darfur

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Sudan (UNMIS) limetoa taarifa yenye kulaani vikali mauaji ya ofisa wa Vikosi vya Amani vya Umoja wa Afrika (AMIS) yalioendelezwa na makundi ya watu wasiojulikana, mnamo tarehe 14 Aprili, kwenye kambi ya wanajeshi iliopo ElFasher.

Mwafaka wa kuacha mapigano Uganda Kaskazini wapongezwa na KM

KM Ban Ki-moon ameyakaribisha makubaliano ya karibuni, kati ya Serekali ya Uganda na waasi wa LRA, ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano mpaka mwisho wa Juni, na pia kuahidi kurejea kwenye mazungumzo ya amani yatakayofanyika kwenye mji wa Juba, 26 Aprili, mazungumzo ambayo yatasimamiwa na Naibu Raisi wa Serekali ya Sudan Kusini. Mazungumzo haya ya amani yalitayarishwa na Joaquim Chissano, Mshauri Maalumu wa KM juu ya mzozo wa Uganda Kaskazini.

WFP imewaomba maharamia kuachia huru mabaharia wa meli yake

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limewaomba wale maharamia walioteka nyara karibuni ile meli iliokodiwa kupeleka chakula Usomali, wawaachie huru mabaharia na chombo chao ili waweze kuendelea kuhudumia kihali ule umma muhitaji wa eneo hilo la Pembe ya Afrika. Meli ya WFP iliyotekwa nyara imeripotiwa kutia nanga katika eneo liliopo karibu na Puntland, Usomali.~

Mkataba wa CITES juu ya udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu

Ofisi Kuu ya taasisi ya Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mimea Pori na Wanyama Wanaohatarishwa Kuangamizwa - mkataba ambao hujulikana kwa umaarufu kama Mkataba wa CITES - hivi karibuni ilichapisha taarifa muhimu yenye kubainisha mapendekezo karibu 40 yanayotakikana yatekelezwe na nchi wanachama ili kurekibisha kanuni za kuendesha biashara ya viumbe pori katika soko la kimataifa.

Mkataba wa CITES juu ya udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu

Ofisi Kuu ya taasisi ya Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mimea Pori na Wanyama Wanaohatarishwa Kuangamizwa - mkataba ambao hujulikana kwa umaarufu kama Mkataba wa CITES - hivi karibuni ilichapisha taarifa muhimu yenye kubainisha mapendekezo karibu 40 yanayotakikana yatekelezwe na nchi wanachama ili kurekibisha kanuni za kuendesha biashara ya viumbe pori katika soko la kimataifa.

Juhudi za kuwasawazishia wanawake haki za kisheria nchini Tanzania

Mnamo 1996, Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Wanawake (UNIFEM) lilidhaminiwa na Baraza Kuu la UM madaraka muhimu ya kusimamia matumizi ya Mfuko wa Amana ulioanzishwa wakati huo Kukomesha Unyanyasaji na Utumiaji Nguvu dhidi ya Wanawake.

ICC kufichua orodha ya majina ya watuhumiwa dhidi ya makosa ya jinai katika Darfur.

Mahakama ya UM juu ya Jinai ya Halaiki (Mahakama ya ICC) imetengaza kuwa itawasilisha mbele ya Mahakama Ndogo, mnamo Februari 27 (2006)orodha ya awali ya majina ya watuhumiwa walioshukiwa kushiriki kwenye vitendo vya uhalifu wa vita na jinai dhidi ya utu katika jimbo la Sudan magharibi la Darfur.

MONUC imethibitisha askari watoto wanaendelea kuajiriwa DRC, kinyume na kanuni za kimataifa

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUC)limethibitisha kwenye ripoti yake iliobainishwa wiki hii, ya kuwa askari watoto, wenye umri mdogo, bado wanaendelea kushinikizwa kusema uongo kuhusu umri wao na hadhi yao ya kiraia, ili wapate fursa ya kujiandikisha na jeshi jipya la muungano la taifa. TRukio hili limeshuhudiwa kujiri katika jimbo la Kivu Kaskazini.

KM akariri mwito wa kuimarisha ushirikiano na Afrika, na kusifu mchango wa Ufaransa katika Afrika

Alkhamisi Mshauri wa KM juu ya Masuala ya Kisiasa, Tuliameni Kalomoh aliwasilisha risala maalumu ya KM Ban Ki-moon kwenye Mkutano Mkuu wa siku tano juu ya hatua za kuimarisha uhusiano kati ya Afrika na Ufaransa uliofanyika kwenye mji wa Cannes, Ufaransa. Viongozi wa kutoka mataifa kadha ya Afrika pamoja na Ufaransa walihudhuria mkusanyiko huo.