Sheria na Kuzuia Uhalifu

UM wachukizwa na kusikitishwa na mauaji ya Benazir Bhutto

KM wa UM Ban Ki-moon aliripotiwa akisema kama alishtushwa na kughadhibiwa, halkadhalika, baada ya kuarifiwa kwamba kiongozi wa Chama cha PPP, na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Benazir Bhutto, aliuawa Alkhamisi kwa bomu la kujitolea mhanga.

MONUC yawataka wapiganaji waasi kusalimisha silaha

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) limetoa mwito uliowahimiza wapiganaji waasi kusitisha mapigano na kusalimisha silaha, na kuchukua fursa hiyo ya baadaye kujiunganisha na mpango wa kitaifa utakaowachanganyisha, kwa utartaibu ulio halali, na maisha ya kawaida ya jamii nchini.

Aliyetoa ushahidi bandia mbele ya Mahakama ya ICTR kuhukumiwa kifungo cha miezi tisa

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imemhukumu kifungo cha miezi tisa jela yule shahidi aliyetambuliwa kwa alama ya jina la GAA, ambaye alituhumiwa kutoa ushahidi usio sahihi mble ya mahakama baada ya kula kiapo.

Mwendesha Mashitaka wa ICC ameishtumu Sudan kukataa ushirikiano na Mahakama

Luis Moreno Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya UM juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) aliwaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kwenye kikao cha hadhara kwamba kwa muda wa miezi 10 sasa Serikali ya Sudan imeshindwa kutekeleza pendekezo la Baraza la Usalama la kuwakamata raia wawili wa Sudan, Ahmad Harun na Ali Kushayb, na kuwapeleka Mahakamani Hague, Uholanzi baada ya raia hawa kutuhumiwa makosa ya jinai ya vita katika Darfur.