Sheria na Kuzuia Uhalifu

MONUC yajaribu kupatanisha makundi yanayohasimiana DRC

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) inajishirikisha katika jukumu, lisio rasmi, la kujaribu kupatanisha vikosi vya serekali vya FARDC na wafuasi wa Jenerali aliyetoroka jeshi, Laurent Nkunda. Huduma hii inafanyika katika jimbo la kaskazini-mashariki ya nchi.

Mjumbe wa UM kwa tatizo la Uganda kaskazini afanyisha mazungumzo ya amani na viongozi husika

Wiki hii Raisi mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano na pia Mjumbe Maalumu wa KM juu ya mzozo wa sugu wa Uganda kaskazini, ameanza kukutana kwa mazungumzo ya amani na viongozi kadha wa eneo, ikiwa miongoni mwa juhudi za kimataifa za kuwasilisha suluhu ya kudumu kati ya makundi yanayohasimiana, yaani Serekali ya Uganda na kundi la waasi la LRA.

Kesi ya jinai ya vita ya Raisi wa zamani wa Liberia kuakhirishwa

Kesi ya makosa ya jinai ya vita dhidi ya aliyekuwa raisi wa Liberia, Charles Taylor imeakhirishwa hadi mwakani na Mahakama Maalumu kwa Sierra Leone baada ya majaji wa Mahakama kuamua kuwapa mawakili wanaomtetea mshitakiwa muda zaidi wa kupitia na kudurusu kwa makini ushahidi.

Kuongezeka kwa ghasia dhidi ya vyombo vya habari huko Somalia

Kwa mara nyingine vyombo vya habari huru huko Somalia vyapoteza waandishi habari wawili mwishoni mwa wiki iliyopita. Ali Iman Sharmarke muanzilishi na mwenyekiti wa kituo mashuhuru cha redio na televisheni pamoja na mwandishi habari wa kipindi mashuhuri Mahad Ahmed Elmi wa kituo hicho hicho, waliuliwa karibu wakati mmoja huko Mogadishu.