Sheria na Kuzuia Uhalifu

Ethopia: mkuu wa haki za binadam wa UM apongeza kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa.

Kamishna mkuu wa haki za binadam wa UM amekaribisha msamaha na kuachiliwa hivi karibuni zaidi ya viongozi wa kisiasa na wakereketwa 30 huko Ethopia na kuhimiza kuwepo na utaratibu wa haki kwa madarzeni ya washtakiwa ambao baado kesi zao hazi kumalizika.

Sierra Leone: Mahakama inayoungwa mkono na UM yatoa hukumu ya kwanza

Mahakama maalum juu ya Sierra Leone inayoungwa mkono na UM imetoa hukumu yake ya kwanza wiki hii, ya vifungo virefu vya jela kwa viongozi watatu wa zamani wa waasi.

Hapa na pale

. Walinda amani wa Jordan katika kikosi cha UM huko Ivory Coast wametoa madawa kwa taasisi ya elimu huko mjini Cocody kama sehemu ya juhudi zao za huduma za dhaura kusaidia taifa hilo lililogawika mapande mawili. Kamanda wa kikosi chao Kanali Ali Bairat alisema msaada huo una lengo la kusaidia kupambana na malaria na ni sehemu ya shughuli za huduma za dharura zinazofanywa na wajumbe wa amani kutoka Jordan, ili kusadia kupunguza maafa kwa raia wa kawaida. ~

UNHCR na IMO yatoa mwito kupunguza vifo baharini

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na shirika la kimataifa la safari za baharini IMO, yameungana kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua zaidi kuzuia vifo vinavyo tokea miongoni mwa watu wanaosafiri kwa maboti katika safari za hatari kabisa kuvuka bahari ya Mediterranean, Ghuba ya aden na kwengineko kujaribu kutafuta maisha bora.

UNICEF yapongeza Misri kupiga marufuku kukeketwa wasichana

Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF limepongeza hatua kadhaa zilizochukuliwa na Misri wiki iliyopita kuondowa mila ya kukeketwa wasichana, baada ya kufariki kwa msichana mwenye umri wa miaka 12 kutokana na kukeketwa.