KM Ban Ki-moon ameyakaribisha makubaliano ya karibuni, kati ya Serekali ya Uganda na waasi wa LRA, ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano mpaka mwisho wa Juni, na pia kuahidi kurejea kwenye mazungumzo ya amani yatakayofanyika kwenye mji wa Juba, 26 Aprili, mazungumzo ambayo yatasimamiwa na Naibu Raisi wa Serekali ya Sudan Kusini. Mazungumzo haya ya amani yalitayarishwa na Joaquim Chissano, Mshauri Maalumu wa KM juu ya mzozo wa Uganda Kaskazini.