Balozi wa kimataifa wa chama cha mpira wa kikapu nchini Marekani, NBA, Dikembe Mutombo amesema kuwapatia vijana elimu inayowawezesha kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani ni suala mujarabu katika kutekeleza lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalohusu amani, haki na taasisi thabiti.