Sheria na Kuzuia Uhalifu

Maharamia wa Kisomali wasiruhusiwe kuwepa adhabu:UM

Kuepuka adhabu kwa maharamia wanaoendesha shughuli zao katika pwani ya Somalia lazima kushughulikiwe kwa kuunga mkono kushitakiwa kwao katika taifa hilo la pembe ya Afrika amesema mshauri wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa kundi la FDLR la Rwanda afikishwa ICC

Taarifa kutoka mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya The Hague zinasema mkuu wa kundi la waasi la Rwanda anayeshutumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefikishwa kwenye mahakama hiyo hii leo na waendesha mashitaka wa Ufaransa .

Wanajeshi wa FARDC wakiuka haki za binadamu

Ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu imearufu kuwa uchunguzi uliofanywa na mpanho wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO na ule uliofanywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu katika vijiji vya Kivu ya Kaskazini na Kivu ya Kusini umetoa mwangaza wa ukiukwaji ulikofanywa na wanajeshi wa serikali wa FARDC wakati wa mwaka mpya.

Ban alaani shambulio la bomu uwanja wa ndege Moscow

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la bomu lililofanyika leo kwenye uwanja wandege wa Domodedovo mjini Moscow Urusi ambalo limekatili maisha ya wengi na kujeruhi wengine.

Maharamia hawakabiliwi na sheria za kimataifa: UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masula ya uharamia Jack Lang amesema kuwa maharamia wengi wa Kisomali wanaaokamatwa kwenye bahari ya Hindi huwa wanaachiliwa bila kufunguliwa mashtaka.

Kamati mpya ya kuchunguza mzozo kati ya Israel na Palestina yateuliwa

Wanachama wapya wa kamati ya wataalamu wa Umoja wa wanakutana mjini Geneva kanzia hii leo kuamua hatua watakazo chukua na kuimarisha mawasilino na pande zingine.

Jamii ya kimataifa yatakiwa kuisadia Somalia:UM

Huku Somalia ikiadhimisha miaka ishirini bila serikali Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa jamii ya kimataifa kujitokeza na kulisaidia taifa hilo lililokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe linapojikakamia kuwahakikishia amani wananchi wake.

Kupekuwa mgari ya UM Ivory Coast ni ukiukaji wa sheria

Umoja wa Mataifa umetoa onyo kwa uongozi wa Icory Coast kutosimamisha na kukagua magari ya Umoja wa Mataifa. Amri ya kufanya upekuzi ilitolewa kwa majeshi yanayomuunga mkono Rais Laurent Gbagbo kupitia vyombo vya habari vya serikali.

Wanawake wanaoshi maeneo ya vijijini wanakabiliwa na ukosefu wa usawa wa kijinsia:UM

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinsia na ajira ya kazi za shambani inaonyesha kuwa wakawake bado wananufaika kwa asilimia ndogo kuliko wanaume katika upande wa ajira katika sehemu za vijijini suala ambalo linachangiwa na hali mbaya ya uchumi na uhaba wa chakula.

Mexico yatakiwa kuchunguza hatma ya wahamiaji waliotekwa

Serikali ya Mexico imetakiwa kuchunguza kisa cha utekaji nyara cha wahamiaji 40 ambao kwa muda wa mwezi mmoja sasa hawajulikani waliko.