Kiongozi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Congo, amepongeza na kukaribisha uamuzi wa mahakama moja ambayo imemkuta na hatia afisa wa jeshi juu ya makosa ya ubakaji na ukiukaji wa haki za binadamu.
Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa juu ya uhalifu Luis Moreno-Ocampo, amesema uamuzi wa kuona haki na usawa unatendeka nchini Libya upo mikononi mwa wananchi wenyewe.
Ripoti mpya iliyotolewa na kamishna wa umoja wa mataifa juu ya haki za binadamu imeainisha maeneo kadhaa ambayo yanaendelea kukwaza misingi ya haki za binadamu nchini Ivory Coast tangu nchi hiyo ifanye duru ya pili ya uchaguzi wa rais.
Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linakutana wiki hii kujadilia
mwenendo wa mambo huko Libya. Mkutano huo ni matokoe ya maombi yaliyowasishwa na Hungary kwa Umoja wa Ulaya na tayari umeungwa mkono na nchi wanachama 44.
Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Navi Pillay ameonya juu ya matumizi ya nguvu nchini Libya kujaribu kuzuia maandamano ya amani akisema kuwa hatua hiyo inaweza kupindukia haki za kibinadmu.
Mahakama moja ya kijeshi nchini Congo imewatupa gerezani askari 8 ambao wamepatikana na hatia ya kuhusika kwenye tukio la ubakaji wa wanawake 50 katika eneo kaskazini mwa nchi hiyo.