Wiki hii wajumbe kutoka nchi 11 za ukanda wa maziwa makuu, wadau wa sekta ya madini na makampuni yanayohusika na biashara ya madini wamekuwa wanakutana mjini Kigali -nchini Rwanda kujadili na kuweka taratibu zitakazohakikisha kwamba madini yanayochimbwa katika nchi za maziwa makuu ni salama , unazingatia mazingira na hauhusishi vikundi vya waasi.