Sheria na Kuzuia Uhalifu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anasema "kashtushwa" na miripuko ya ghasia katika Iran

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu kwenye taarifa aliotoa kwa vyombo vya habari Ijumatano alisema ya kuwa alishtushwa na kile alichokiita "mfumko wa vifo, majeraha na watu kukamatwa" katika Jamhuri ya KiIslam ya Iran.

UM imelaumu vikali waasi wa LRA kwa mauaji na mateso ya raia katika JKK

Vile vile hii leo, kumewasilishwa ripoti nyengine ya apmoja ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) na Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC) kuhusu mashambulio ya kikatili yaliofanywa na waasi wa LRA katika JKK.

OHCHR inasema mashambulio ya LRA Sudan Kusini ni "madhambi yanayokiuka ubinadamu"

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) Ijumatatu imechapisha ripoti mpya juu ya Sudan, ilioeleza ya kwamba mashambulio katili, dhidi ya raia, yalioendelezwa na wapiganaji waasi wa Uganda wa kundi la LRA katika Sudan Kusini, ni vitendo vilivyofananishwa "sawa na makosa ya jinai dhidi ya ubinadamu."

Mtetezi wa Haki za Binadamu Sahara Magharibi aruhusiwa kurejea nchini

Taarifa iliotolewa na KM Ban Ki-moon, baada ya saa sita za usiku ya Ijumaa, imeeleza kuwa amefarajika na pia kupata nafuu baada ya kupokea ripoti ilioleza mtetezi wa uhuru wa taifa la Sahara ya Magharibi, Aminatou Haidar, aliruhusiwa kurejea kwao kwenye mji mkuu wa Laayoun.

Mkutano wa Cartagena umepitisha azimio la kukomesha mateso ya silaha zilizotegwa

Kwenye Mkutano Mkuu wa Mapitio juu ya Ulimwengu Huru dhidi ya Silaha za Mabomu Yaliotegwa Ardhini, unaofanyika kwenye mji wa Cartagena, Colombia, Mataifa Wanachama yalioidhinisha na kuridhia Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu Yaliotegwa, yameahidi tena kukomesha usumbufu na madhara yanayoletwa na silaha hizo.

Siku ya Kimataifa ya Kuondoshwa Utumwa kuhishmiwa na UM

Tarehe ya leo, Disemba 02 (2009) huhishimiwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Uondoshaji wa Utumwa.

ICC imerekibisha tena uamuzi wa kuachiwa kwa muda Bemba

Mapema Ijumatano Korti Ndogo ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), iliopo Hague, Uholanzi imebatilisha uamuzi wa siku za nyuma wa kumwachia Jean-Pierre Bemba kutoka kizuizini.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa IAEA aanza kazi rasmi Vienna

Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) ameanza kazi rasmi, hii leo, Ijumanne mjini Vienna. Kwenye taarifa kwa waandishi habari ameeleza ya kuwa "mazingira yaliozikabili shughuli za taasisi yao kwa sasa ni ya zahma tupu."

FAO kupitisha mkataba wa kihistoria kudhibiti uvuvi haramu

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limepitisha mkataba mpya wenye lengo la kupiga marufuku vyombo vyote vya baharini na meli zilizoshiriki kwenye uvuvi haramu, kutoegesha kwenye bandari za Mataifa Wanachama.

Siku ya Kimataifa Kufyeka Utumiaji Mabavu dhidi ya Wanawake

Tarehe ya leo, Novemba 25 (2009) inaadhimishwa rasmi na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa Kufyeka Matumizi ya Nguvu na Mabavu dhidi ya Wanawake.