Sheria na Kuzuia Uhalifu

Jumuiya ya kwanza ya mawakili wanawake Usomali kusaidiwa na UNDP

Karibuni, Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) limeisaidia Usomali kuanzisha jumuiya ya kwanza ya mawakili wanawake katika jimbo la Somaliland. ~

Tume ya waliotoweka bila khiari duniani inakutana Argentina

Tume ya Utendaji ya UM juu ya Watu Waliolazimishwa Kutoweka na Kupotea Bila Khiari inakutana katika mji wa Buenos Aires, Argentina kuanzia Julai 24 mpaka 26 kufanya mapitio ya kesi za watu 300 waliotoweka duniani, kuambatana na matatizo ya kisiasa. Tume hiyo ina wajumbe wataalamu watano na inakutana, kwa mara ya kwanza katika taifa la Amerika ya Latina la Argentina, taifa ambalo katika miaka ya sabini na mwanzo wa miaka ya themanini liliathirika sana na tatizo la kupotea kwa wapinzani wingi wa kisiasa, bila ya aila zao kujua walipo.

Ndege zilizobeba madawa ya kulevya zimekamatwa Guinea-Bissau

Kwenye taarifa iliotolewa na Shola Omoregie, Mjumbe wa KM kwa Guinea-Bissau iliripoti kushikwa kwa ndege mbili na watu wa usalama nchini Guinea-Bissau, ndege ambazo zinatiliwa shaka zimebeba shehena ya madawa ya kulevya. Kwa mujibu wa ripoti, baadhi ya watu wanaohusika na ndege hizo wamewekwa kizuizini kwa sasa wakisubiri matokeo ya uchunguzi juu ya fungamano walionayo na biashara ya madawa ya kulevya.

Kukamatwa kwa Karadzic kwasherehekewa na UM dhidi ya uhuru wa kupona adhabu

Mnamo Ijumatatu ya tarehe 21 Julai (2008) Radovan Karadzic, aliyekuwa Raisi wa Republika Srpska wakati wa vita katika Bosnia-Herzegovina, alishikwa na watu wa usalama wa Serbia. Karadzic alikamatwa baada ya kujificha kwa muda wa miaka 13 na kukwepa sheria yakimataifa iliomshitaki katika Julai 25, 1995 kuwa alihusika na mauaji ya halaiki dhidi ya watu wasio Waserb katika Bosni-Herzegovina, ikijumuisha WaBosnia walio Waislamu na Wacroat.

KM na Mwendesha Mashitaka wa ICTY waipongeza Serbia kwa kumshika R. Karadzic

KM wa UM Ban Ki-moon, kwenye taarifa iliotolewa kupitia msemaji wake, alinakiliwa akisema kushikwa kwa Radovan Karadzic kilikuwa ni kitendo cha "kihistoria, hasa kwa waathiriwa" wa jinai ya vita aliyotuhumiwa kuiongoza manjo huyo alipokuwa mkuu wa Waserb katika Bosnia-Herzegovina.

Hapa na pale

Warsha maalumu pamoja na tafrija mbalimbali zinafanyika Makao Makuu ya UM kuadhimisha miaka 10 tangu Sheria ya Roma ilipoidhinishwa na kuanzishwa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC). KM Ban Ki-moon alisema kuanzishwa kwa Mahakama ya ICC ni moja ya mafanikio makubwa ya karne iliopita.~

Uamuzi wa ICC kuilazimisha UNAMID kuhamisha wafanyakazi Darfur

UM inajiandaa hivi sasa kukabiliana na athari za uamuzi wa Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiaki (ICC) ambaye alituma ombi rasmi kwa tume ya majaji watatu la kumshika Raisi Omar Hassan Ahmad AlBashir wa Sudan, aliyetuhumiwa kushiriki kwenye makosa ya vita na jinai dhidi ya utu pamoja na mauaji ya halaiki katika Darfur.

Mahakama ya Makosa ya Vita Sierra Leone iwe funzo kwa kesi za viongozi wakosa

Stephen Rapp, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama maalumu ya Jinai ya Vita katika Sierra Leone aliwaambia waandishi habari kwamba kesi ya kumhukumu aliyekuwa Raisi wa Liberia Charles Taylor inaendeshwa kwa utaratibu wa kufanyiwa mfano, ambao utawafalia wanasheria kuusoma ili kuona namna haki inavyotekelezwa katika sheria za kimataifa kwa viongozi waliokiuka mipaka wakati wakitawala. Alidai kwamba kesi ya mtuhumiwa aliyekuwa raisi wa Liberia, inaonyesha kwamba kesi kama hizo zinaweza kuendeshwa kwa uwazi, bila ya upendeleo, na hata kumpatia mtuhumiwa fursa halali ya kujitetea. ~~

CITES inakutana Geneva kusailia biashara ya pembe na mbao adimu

Mkutano wa UM wa kikao cha 57 cha Kamati Ndogo juu ya utekelezaji wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa kuhusu Udhibiti wa Aina za Wanyama na Mimea Pori Inayohatarishwa Kuangamia (CITES) unafanyika Geneva wiki hii, kuanzia tarehe 14 Julai hadi 18 kuzingatai ombi la Uchina kuruhusiwa kuagizishia tani 100 za pembe za ndovu kutoka Afrika, akiba ambayo imevumbikwa sasa hivi kwenye maghala ya nchi nne za Kusini ya Afrika.

Ofisa wa ICC aelezea UA kesi za mahakama

Fatou Bensouda, Naibu Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) ameripoti Ijumaa mbele ya Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika (UA) mjini Addis Ababa, Ethiopia fafanuzi za mahakama kuhusu maendeleo kwenye zile kesi zenye kusimamiwa na taasisi yao, ikijumuisha pia zile kesi zinazofungamana na mzozo ulioselelea Darfur, Sudan. ~~