Sheria na Kuzuia Uhalifu

Haki za washitakiwa na waliowekwa vizuizini zinazingatiwa na mkutano wa Nairobi

Wawakilishi 150 ziada kutoka nchi 71 wamekusanyika Nairobi, Kenya wiki hii kuhudhuria mkutano wa UM unaozingatia majukumu ya taasisi za kitaifa zilizobuniwa kulinda na kutekeleza haki za binadamu, kwa kulingana na vyombo vya mahakama, utekelezaji wa sheria na uangalizi wa hali kwenye vituo vya kufungia watu.

UNICEF inasailia kampeni ya kukomesha mila ya kutahiri watoto wa kike Mauritania

Wiki hii Alpha Diallo wa kutoka Redio ya UM Geneva alifanya mahojiano maalumu na Christian Skoog, Mwakilishi wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) aliopo Mauritania. Walisailia hali ya watoto nchini humo, kwa ujumla.

Madai ya Georgia dhidi Urusi yapewa usikizi na Mahakama ya ICJ

Mahakama Kuu ya Kimataifa (ICJ) iliopo Hague, Uholanzi ilitazamiwa leo kutoa maamuzi yake juu ya madai ya Georgia ya kwamba Urusi ilikiuka kanuni za kimataifa kwa kuingiza vikosi vyake kwenye jimbo la Ossetia Kusini mnamo tarehe 07 Agosti mwaka huu.

'Msiba mwengine wazuka Ghuba ya Aden': UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuwa imejumuika na washiriki wengine wa kimataifa kuwatafuta wahamiaji karibu 100 wanaoripotiwa kupotea katika Ghuba ya Aden, baada ya kulazimishwa na wafanya magendo kuchupa kutoka kwenye chombo walichokuwemo, nje ya mwambao wa Yemen.

Ngirabatware amekana makosa ya jinai ya halaiki Rwanda

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imeripoti ya kwamba Augustin Ngirabatware, aliyekuwa Waziri wa Mipango ya Nchi Rwanda Ijumaa alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kukabili mashitaka alikana makosa kumi ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki nchini mwao katika miaka ya 1990, jinai ambayo inasemekana ilikiuka sheria ya kiutu ya kimataifa.

Waziri wa zamani Rwanda ahamishiwa kizuizini Arusha

Waziri wa zamani wa Miradi ya Nchi Rwanda, Augustin Ngirabatware, anayekabili mashitaka ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki na ukiukaji mbaya wa kanuni za kiutu za kimataifa, Ijumatano amehamishwa kutoka Frankfurt, Ujerumani, alipokamatwa wiki mbili zilizopita, na kupelekwa kwenye Kituo cha Kufungia Watu cha Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) kilichopo Arusha, katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu ahimiza hifadhi bora kwa wageni Afrika Kusini baada ya mauaji katili

Navanethem Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR), amelaani vikali mauaji ya kikatili yaliotukia Ijumaaa iliopita katika kijiji cha Eastern Cape, Afrika Kusini ambapo Sahra Omar Farah, mama wa KiSomali pamoja na watoto wake wawili wa kiume wajane, ambao mmoja wao alikuwa kiziwi, na vile vile binti wake wa miaka 12 waliuawa kikatili kwa visu na marungu karibu na duka liliokuwa linaendeshwa na Msomali.

IOM itapanua huduma za kuokoa watoto waliotoroshwa Afrika Magharibi

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limetangaza leo kwamba litapanua zaidi mradi wa kusaidia kurejesha makwao wale watoto waliotekwa nyara Afrika Magharibi, na ambao hushirikishwa kwenye kazi za kulazimisha katika nchi za kigeni. Mradi huu ulianzishwa mwaka 2006, na unafadhiliwa na Idara ya Masuala ya Mambo ya Nje ya Marekani.