Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mwendesha Mashtaka wa ICC awasiliana na viongozi wa kimataifa juu ya Darfur

Luis Moreno Ocampo, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) yupo New York kwa madhumuni ya kuwasiliana na watendaji wa kimataifa – yaani UM na wawakilishi wa Afrika – kuhusu taratibu za kuwapatia raia wa Darfur hifadhi ziada na kukomesha vitendo vya uhalifu dhidi yao na kuhakikisha maamuzi na madaraka ya Mahakama juu ya suala hilo yanatekelezwa haraka kwenye eneo la mtafaruku la Sudan magharibi.

Nchi 17 zakubali mapendekezo ya kudhibiti kisheria vitendo vya makampuni ya wanajeshi wa kukodi

Wataalamu kutoka nchi 17 waliokutana kwenye kikao maalumu kwenye mji wa Montreux, Uswiss kuanzia Ijumatatu (15/09/08), kuzingatia udhibiti bora wa shughuli za yale makampuni ya wanajeshi wa binafsi wanaohudumia usalama, hii leo wamepitisha warka maalumu uliosisitiza ya kuwa Serikali za Mataifa zina dhamana kuu ya kuhakikisha askari wakandarasi wa binafsi wanaokodiwa kushiriki kwenye maeneo ya uhasama na vita huwa wanafuata sheria za kiutu za kimataifa.

Matumizi ya madawa ya usanisi yameshuhudiwa kuongezeka katika nchi zinazoendelea, UNODC yaripoti

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) imebainisha kwenye ripoti ya \'Tathmini ya 2008 juu ya Madawa ya Kulevya Yanayotumiwa kama Viburudisho Duniani\' kwamba matumizi ya yale madawa ya usanisi ya anasa – kama "amphetamine, metamphetamine (meth) na ecstasy" – yamebainika kuzidi katika nchi zinazoendelea, hasa katika maeneo ya Mashariki na Kusini-Mashariki ya Bara la Asia na katika Mashariki ya Kati.

UM umeitisha mjadala maalumu kusikiliza hisia na maoni ya waathiriwa wa ugaidi duniani

Hii leo, kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, kumeanzishwa mjadala maalumu wa kihistoria, ulioandaliwa na KM Ban Ki-moon mwenyewe, ambao umewakusanyisha waathiriwa wa vitendo vya ugaidi kutoka sehemu kadha za kimataifa na kuwapatia fursa ya kuelezea hisia zao juu ya misiba waliopitia, kwa madhumuni ya kuwakilisha taswira ya kiutu kwa waathiriwa wa janga la ugaidi duniani.

Usafirishaji wa magendo warejea tena kwenye Ghuba ya Aden

Baada ya kurudi kwa hali shwari kwenye Ghuba ya Aden imeripotiwa na hirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kuanza tena, upya, mnamo mwezi Agosti, usafirishaji magendo wa wahamiaji waliokuwa wakijinusurisha na njaa pamoja na mapigano katika eneo la Pembe ya Afrika, hususan wahamiaji kutoka Usomali na Ethiopia.

Uharamia Usomali wamtia kiherehere Mjumbe wa KM

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmmedou Ould Abdallah amesema ameshtushwa sana kwa kuongezeka kwa uharamia kwenye mwambao wa Usomali, kitendo ambacho alisisitiza kinahatarisha utulivu kurejea kwenye eneo hilo la Pembe ya Afrika.