Sheria na Kuzuia Uhalifu

Makao Makuu yawakumbuka na kuwaheshimu waathiriwa wa utumwa

Kuanzia Ijumanne ya leo, tarehe 25 Machi, UM umeanzisha taadhima za karibu wiki moja za kuwakumbuka waathiriwa wa janga la utumwa pamoja na kuadhimisha siku Biashara ya Utumwa kwenye ngambo ya Bahari ya Atlantiki ilipositishwa na Marekani miaka mia mbili iliopita.

Bukini imetia sahihi ya kuridhia Mkataba wa Roma

Mapema wiki hii taifa la Bukini limetia sahihi ya kuridhia Mkataba wa Roma, ambao ndio ulioanzisha Mahakama ya Kimataifa ya ICC. Mahakama ya ICC ni mahakama huru na ya kudumu, iliyodhaminiwa na jumuiya ya kimataifa madaraka ya kuhukumu wale watu waliotuhumiwa kufanya makosa mabaya ya jinai, mathalan, mauaji ya halaiki, jinai ya vita na vile vile yale makosa ya uhalifu dhidi ya utu.

Mahakama ya ICTR kuongeza hukumu kwa padri wa zamani Rwanda

Mahakama ya Rufaa ya ile Mahakama Kuu ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) iliopo Arusha, Tanzania imerekibisha hukumu yake ya hapo kabla na kuongeza adhabu kwa aliyekuwa padri wa madhehebu ya Kikatoliki nchini Rwanda, Athanase Seromba ambaye katika mwaka 2006 alihukumiwa kifungo cha miaka 15, kwa kusaidia na kuchochea mauaji ya karibu raia 1,500 wenye asili ya KiTutsi ambao katika 1994 walikimbilia ndani ya kanisa alikuwa akiliongoza kupata hifadhi katika mkoa wa Kibuye.

ICC kuendesha kesi mbili kwa pamoja za watuhumiwa wa jinai ya vita katika JKK

Majaji wa Mahakama ya UM juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) iliopo mjini Hague, Uholanzi wameamua kuendesha kesi mbili, baadaye mwaka huu, kwa wakati mmoja, zinazowahusu viongozi wawili waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), yaani Germain Katanga na Mathieu Ngudjolo Chui, ambao walituhumiwa kuendeleza makosa ya vita na jinai dhidi ya utu katika eneo la mashariki ya taifa hilo, mnamo 2003. Miongoni mwa mashitaka waliokabiliwa nayo watuhumiwa hawa ni pamoja na kushtakiwa kushiriki kwenye mauaji ya mamia ya watu na kuendeleza karaha ya kunajisi wanawake kimabavu katika jimbo la Ituri.~

UNODC yatahadharisha:'tatizo la madawa ya kulevya limedhibitiwa lakini halijasuluhishwa.'

Antonio Maria Costa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) alipohutubia kikao cha 51 Kamisheni ya UM dhidi ya Madawa ya Kulevya kilichokutana Ijumatatu Vienna – taasisi ambayo huzingatia sera za kukomesha janga la madawa haribifu duniani – alisema kwamba wakati umeshawadia kwa jumuiya ya kimataifa kuzingatia hatua ziada za kudhibiti vyema afya ya watu waliodhurika na madawa maovu badala ya kulenga huduma zake kudhibiti uhalifu pekee wa madawa ya kulevya.

Watoto waliotoroshwa Chad kurejeswha kwa aila zao

Watoto 100 ziada, wingi wao wakiwa raia wa Chad, ambao miezi mitano iliopita walitaka kutoroshwa na kupelekwa nje na shirika wahisani la Kifaransa la Zoe’s Ark, wanatazamiwa kurejeshwa kwa wazee wao mnamo siku za karibuni.

Rwanda yakubali kupokea wahalifu waliohukumiwa na ICTR

Mapema wiki hii mjini Kigali, Adam Deng, Msajili wa Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, walitia sahihi maafikiano ya kupeleka kifungoni kwenye magereza ya Rwanda wale watu waliohukumiwa adhabu na Mahakama. Rwanda itakuwa ni taifa la saba kuidhinisha huduma ya kuweka vizuizini wale watu waliohukumiwa na Mahakama ya ICTR kushiriki kwenye jinai ya halaiki katika Rwanda.