Habari Mpya

ICTR yahukumu kifungo cha miaka 15 kwa aliyekuwa padri Rwanda

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imepitisha hukumu ya kifungo cha jela cha miaka 15 kwa Athanase Seromba aliyekuwa padri wa Parokia ya Nyange katika kijiji cha Kivumu magharibi ya Rwanda.

Chuo Kikuu cha Pretoria kutunukiwa zawadi ya UNESCO

Kitivo cha Haki za Kiutu cha Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini kinachosimamia mafunzo yanayohusu taratibu za kuimarisha haki za kimsingi kimetunukiwa zawadi ya dola 10,000 na Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Ripoti juu ya juhudi za karibuni kupiga vita malaria

Hivi karibuni takwimu za UM zilithibitisha ya kuwa watu milioni 300 hadi 500 huambukizwa maradhi ya malaria duniani, kila mwaka, na kati ya idadi hiyo watu milioni 1 hufariki, asilimia kubwa yao ikiwa watoto wachanga kutoka bara la Afrika.

Juhudi za Baraza Kuu kudhibiti biashara haramu ya almasi.

Mnamo mwanzo wa wiki Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio la kuunga mkono Mpango wa Kimberley na kupendekeza utaratibu huo uendelea kuimarishwa kimataifa. Kabla ya azimio kupitishwa Mataifa Wanachama 192 wa UM walisikia ripoti ya mapitio kutoka Raisi Festus Gontebanye Mogae wa Botswana, Mwenyekiti wa mwaka huu wa nchi zilizoridhia na kuidhinisha Mpango wa Kimberley.

Vurugu la Darfur huenda likaathiri mataifa jirani aashiria KM

KM wa UM ameelezea kuchukizwa sana kwa kufumka tena, hivi karibuni, katika jimbo la magharibi la Sudan la Darfur, vurugu na wasiwasi. Hali hiyo ilisababisha idadi kubwa ya raia wa Darfur kuhajiri maskani yao ili kunusurisha maisha.

UM kupunguza wahudumia misaada ya kiutu katika Chad

UM umetangaza kwamba kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuharibika katika eneo la Chad ya mashariki zile huduma za kupeleka misaada ya kihali kwa wahamiaji wa Sudan 110,000 waliopo huko zitabidi zipunguzwe pamoja na kupunguza wafanyakazi wa UM wanaohusika na kadhia hizo.

Jumuiya ya Kimataifa Yaadhimisha 'Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani'

Mnamo 1988 Baraza Kuu la UM lilitoa mwito maalumu uliopendekeza kuutekeleza uamuzi wa Shirika la Afya Dunia (WHO) wa kuifanya tarehe 01 Disemba kila mwaka kuwa ni ‘Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani.’

Mapigano makali Sudan ya kusini yaharamisha maafikiano ya amani, ashtumu KM

KM Kofi Annan ameripotiwa kushtumu yale mapigano makali yalioshtadi hivi majuzi katika mji wa Malakal, uliopo katika Jimbo la Nile ya Juu, Sudan ya Kusini, uhasama uliozuka kati ya Jeshi la Serekali ya Sudan (SAF) na kundi la waasi la SPLA. Kitendo hiki, alisisitiza KM, kiliharamisha kihakika na kukiuka yale Maafikiano ya Jumla ya Amani.

Waathiriwa wa mafuriko Ethiopia wapelekewa misaada ya dharura na UM

UM wiki hii umeongeza huduma zake za kusafirisha kwa ndege misaada ya chakula na madawa katika eneo la kusini-mashariki ya Ethiopia.

Mshoni wa Zambia kutunikwa zawadi ya UM kwa kupiga vita UKIMWI

Jonsen Habachimba, mshoni kutoka Zambia pamoja na shirika linalojulikana kama Jumuiya ya Maendeleo ya Vijiji ya Mboole (Mboole Rural Development) wametunukiwa zawadi ya dola 20,000, ikiwa ni tunzo la awali la UM kwa mashirika ya kiraia yanayojitolea kushiriki kwenye juhudi muhimu za kupambana na UKIMWI.