Habari Mpya

UNHCR kuharakisha operesheni za kurudisha wahamiaji Sudan ya kusini

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuongeza kasi kwenye operesheni zake za kuwarudisha makwao wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPS) wa eneo la Blue Nile, Sudan ya kusini.

Makundi husika na mzozo wa Darfur yakiri vurugu halizalishi suluhu, wabainisha Wapatanishi wa UM na AU

Jan Eliasson, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Darfur pamoja na Salim Ahmed Salim, Mpatanishi wa Darfur wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) walikutana wiki hii nchini Sudan kwa mashauriano ya amani na viongozi wa wahamiaji wa ndani ya nchi, majemadari wa makundi ya waasi wasiotia sahihi Itifaki ya Amani ya Darfur, pamoja na machifu wa makabila kadhaa na vile vile wawakililishi wa Sereklali.

Watoto masikini na mayatima Zimbabwe kufadhiliwa misaada ya maendeleo na UM

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wiki hii limetiliana sahihi na Serekali ya Zimbabwe, pamoja na mashirika 21 yasio ya kiserekali, maafikiano ya kufadhilia jumuiya za kiraia misaada ya kuhudumia uandikishaji ziada wa watoto masikini na mayatima 350,000, ili waweze kuhudhuria masomo ya skuli za msingi. Vile vile msaada huo unatazamiwa kuwahudumia afya na kuboresha lishe watoto husika.

KM Ban Ki-moon ameliarifu Baraza la Usalama juu ya ziara yake Afrika

Mapema wiki hii KM Ban Ki-moon alikutana na wajumbe wa Baraza la Usalama, kwenye kikao cha faragha, na walizingatia matokeo ya mazungumzo aliyokuwa nayo KM na viongozi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) walipokutana kwenye pambizo za Mkutano Mkuu uliofanyika karibuni katika mji wa Addis Ababa, Ethiopia.

Naibu KM mpya aahidi usimamizi wa kazi za UM kwa nidhamu za fungamano

Ijumatatu, Februari 05 (2007) Asha-Rose Migiro, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo wa Tanzania aliapishwa rasmi kuwa Naibu KM mpya wa UM. Baada ya Bi Migiro kuapishwa na kutia sahihi waraka za UM alijulishwa na KM Ban Ki-moon na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Naibu KM Migiro aliwaambia wanahabari hawo kwamba atajitahidi kama awezavyo kuziongoza kazi za UM kwa nidhamu iliyoungana, na kwa taratibu zinazoeleweka kwa masilahi na natija za taasisi hii pekee ya kimataifa.

Maelfu wanahitajia misaada ya kihali kusini Afrika baada ya mafuriko haribifu

Shirika la WFP limeripoti mafuriko haribifu yametanda karibuni kusini ya Afrika na kuathiri maisha na usalama wa makumi elfu ya watu waliojikuta wamenaswa na kuinuka kwa kina cha maji katika maeneo yao,hali ambayo imeangamiza mazao, nyumba na kuchukua maisha ya darzeni za watu.

Mataifa Wanachama yakutana mjini Paris kuzingatia ukomeshaji wa matumizi ya watoto katika mikwaruzano ya vita

Mnamo mwanzo wa wiki wawakilishi kutoka mataifa wanachama 58 walikutana kwa siki mbili katika mji wa Paris, Ufaransa kwenye mkutano uliopitisha itifaki ya kukomesha, kote ulimwenguni, tabia karaha na vitimbi haramu vya kuajiri kwa nguvu watoto wanaolazimishwa kushiriki katika vita na mapigano.

Watoto milioni 4.5 Ghana watapatiwa matibabu dhidi ya minyoo

Wiki ijayo UNICEF, ikishirikiana na idara za ilimu na afya katika Ghana wanatarajiwa kujumuika kuanzisha huduma za siku nne zenye dhamira ya kuwapatia watoto milioni 4.5 waliopo katika skuli za serekali 28,000, matibabu dhidi ya maradhi ya minyoo.

Juhudi za kimataifa za kuboresha maisha kwa wakazi wa mitaa ya mabanda Afrika Mashariki (Sehemu ya Pili)

Mwandishi habari wa Redio ya UM, Michele Montas hivi majuzi alizuru mtaa wa mabanda wa Mathare katika vitongoji vya Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Juhudi za kimataifa za kuboresha maisha kwa wakazi wa mitaa ya mabanda Afrika Mashariki (Sehemu ya Kwanza)

Hivi karibuni, aliyekuwa mwandishi habari wa Idhaa ya Redio ya UM, Michele Montas alizuru Kenya kuangalia namna mashirika wenzi na UM yanavyoendeleza huduma za kupunguza umasikini, hasa miongoni mwa ule umma wenye kuishi kwenye mazingira ya hali duni.