Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet ameelezea hofu yake juu ya kuendelea kwa ukosefu wa uwazi kuhusiana na vifo na matibabu ya watu 7,000 wanaoshikiliwa nchini Iran, wakati huu ambapo msako unaripotiwa kuendelea katika taifa hilo.