Nataliia Vladimirova alikimbia nyumbani kwake Kharkiv, Ukraine, siku ya kwanza tu Urusi ilipovamia nchi yao tarehe 24 mwezi Februari, 2022, akiambatana na binti yake Oleksandra mwenye umri wa miaka 4 pamoja na mama mkwe wake. Wao ni miongoni mwa maelfu ya wakimbizi wa Ukraine waliopata hifadhi ya muda nchini Ureno . Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Ureno, Nataliia al maaruf Natasha, anasimulia simulizi wa yale aliyopitia ikiwemo kugawanyika kwa familia sambamba na kupoteza wengine.