Msaada wa Kibinadamu

Holmes ainasihi Zimbabwe kuondoa vikwazo dhidi ya wagawaji misaada

Mshauri wa UM juu ya Misaada ya Dharura, John Holmes, ameiomba Serikali ya Zimbabwe kuondosha vikwazo dhidi ya mashirika yasio ya kiserikali yaliopo nchini humo, kwa sababu vikwazo hivyo vinaathiri hali za watu milioni 2 nchini humo wanaotegemea misaada ya kimataifa kumudu maisha.

UNICEF imetoa mwito wa dharura wa kuisaidia Ethiopia kukabili tatizo la utapiamlo

Hilde Johnson, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) aliwaambia wafadhili wa kimataifa mjini Geneva mnamo 26 Juni (2008) kwamba hali ya watoto katika Ethiopia ni ya kushtusha sana na ya hatari, kutokana na ukame uliotanda nchini humo kwa muda mrefu ikichanganyika pamoja na matatizo ya kupanda kwa bei za chakula.

Darfur inakabiliwa na janga la kiutu "timilifu", mashirika ya UM yaonya

Mashirika ya UM yaliopo kwenye eneo la Sudan magharibi la Darfur limetahadharisha kwenye taarifa iliotolewa ya pamoja kwamba hali iliojiri Darfur sasa hivi inaelekea kuzusha "dhoruba timilifu" ya matatizo ya kiutu, hususan yale matatizo yanayoambatana na upungufu wa chakula, halia ambayo imekorogwa zaidi kwa sababu ya kuongezeka kwa fujo na vurugu kieneo, na pia kufurika kwa kambi za umma uliong\'olewa makwao, ikichanganyika na mavuno haba katika mwaka huu.

Siku ya Wahamiaji Duniani Inaadhimishwa Kimataifa

Tarehe 20 huadhimishwa kila mwaka kimataifa, kuwa ni Siku ya Wahamiaji Duniani – siku ambayo umma wa kimataifa huheshimu na kukumbushana juu ya jukumu liliodhaminiwa Mataifa Wanachama na Mkataba wa UM kuhudumia kihali na mali umma wenziwao uliong\'olewa kwa nguvu makwao kwa sababu wasioweza kuzidhibiti. Kadhalika mnamo siku hiyo walimwenngu huheshimu mchango wa wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa wanaoshughulikia ugawaji wa misaada ya kiutu kwa wahamiaji hawo.

Siku ya Wahamiaji Duniani kuadhimishwa kwa nasaha ya kuhifadhi bora waliong'olewa makwao

Tarehe 20 Juni inaadhmishwa kila mwaka kuwa ni Siku ya Wahamiaji Duniani, siku ambayo jumuiya ya kimataifa hukumbushana juu ya masaibu yanayowapata wahamiaji na wakimbizi wa kimataifa, na kushauriana taratibu za kuwahudumia watu waliong\'olewa makwao kihali na mali ili waweze kushiriki tena kwenye maisha ya kawaida. Jennifer Pagonis msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Geneva aliwapatia waandishi habari wa kimataifa Geneva sababu zilizoihamasisha jamii ya kimataifa kuidhamisha siku hiyo.~~Sikiliza habari kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Zimbabwe inahitajia huduma za kimataifa kukidhi mahitaji ya umma

John Holmes, Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) Alkhamisi aliwaambia waandishi habari hapa Makao Makuu kwamba hali katika Zimbabwe inazidi kuharibika na anakhofia mavuno yajayo hayatomudu kukidhi mahitaji ya chakula kwa robo tatu ya watu nchini.

Ukame uliokithiri Ethiopia wailazimisha OCHA kuomba msaada ziada

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ikijumuika na mashirika mengine ya UM na Serikali ya Ethiopia, yameripoti kwamba wamelazimika kuomba waongezewe misaada ya dharura na wahisani wa kimataifa kwa sababu ya kujiri kwa hali mbaya ya ukame Ethiopia. Msaada huo unatakiwa kuwahudumia chakula mamilioni ya waathiriwa wa ukame ambao idadi yao katika siku za karibuni ilikithiri kwa kiwango kikubwa kabisa.

Upungufu wa fedha kuilazimisha WFP kupunguza shughuli Sudan

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba litalazimika kupunguza huduma zake za anga, zinazotumiwa kugawa misaada ya chakula kwa umma muhitaji katika eneo la mgogoro la Darfur, na kwenye sehemu nyengine zilizotawanyika masafa kadha wa kadha nchini Sudan.

Mshauri wa KM anazuru eneo la Sahel kutathminia hali

Jan Egeland, Mshauri Maalumu wa KM ameanza ziara ya siku tano kuyatembelea mataifa ya Sahel mapema wiki hii. Ijumatatu alikuwepo Burkina Faso ambapo alinakiliwa akisema kwamba eneo la Sahel ni kama ‘ardhi chimbuko’ yenye kufukuta mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha mizozo aina kwa aina, hali ambayo inahitajia kudhibitiwa haraka, aliongeza kusema.

Utaalamu na mahema kufadhiliwa Afrika Kusini na UNHCR kwa waathiriwa wa hujuma za chuki

Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Geneva, Ron Redmond alipokutana na waandishi habari wa kimataifa Ijumaa aliripoti ya kuwa taasisi yao imepeleka misaada ya dharura Afrika Kusini itakayochangia juhudi za Serikali katika kuwahudumia kihali maelfu ya waathiriwa wageni waliong\'olewa makwao baada ya kushambuliwa kibaguzi karibuni nchini humo.~