Msaada wa Kibinadamu

Mratibu wa UM juu ya huduma za kiutu ahimiza misaada ziada kunusuru Wasomali na "ufukara uliotota"

Mratibu wa UM juu ya Misaada ya Kiutu kwa Usomali, Mark Bowden, kwenye mahojiano na waandishi habari wa kimataifa, yaliofanyika Makao Makuu, Ijumatano alasiri, alihadharisha kwamba bila ya wahisani wa kimataifa kuchangisha misaada ya dharura inayotakiwa kuuvua umma wa Usomali na mgogoro unaohatarisha maisha yao, kunaashiriwa idadi kubwa ya raia watakabiliwa na “ufukara kamili, wa kutota.”

UM waomba ufadhiliwe dola bilioni 2.2 kuhudumia Sudan

UM umetangaza ombi maalumu la kutaka ifadhiliwe dola bilioni 2.2 kuhudumia misaada ya kiutu katika Sudan.

UM umetangaza ombi la kutaka ufadhiliwe dola bilioni 7 kuhudumia kidharura watu milioni 30 katika 2009

Ijumatano KM Ban Ki-moon amewasilisha mjini Geneva, waraka maalumu wenye ombi linalotaka jamii ya kimataifa ifadhilia UM msaada wa dola bilioni 7 ili kushughulikia huduma za dharura, za kiutu, katika 2009, kwa watu milioni 30 wanaoishi katika nchi 31 duniani.

Wahudumia misaada ya kiutu Lubero Kusini wasitisha shughuli kutokana na ukosefu wa usalama

Ofisi ya UM inayohusika na Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mashirika yenye kuhudumia misaada ya kiutu katika eneo la mapambano la JKK, hasa katika Lubero Kusini, yamelazimika kuhamisha wafanyakazi wao kwa sababu ya kutanda kwa hali ya wasiwasi kieneo.

WFP yakamilisha ugawaji chakula Kongo mashariki kwa wahamiaji 135,000

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kukamilisha ugawaji wa posho ya siku kumi kwa wahamiaji muhitaji 135,000 ambao waling’olewa makazi kwa sababu ya mapigano.

UNHCR yaendelea kuhudumia kihali wahamiaji wa dharura Goma

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) nalo pia linaendelea na juhudi za kuwahudumia kihali maelfu ya wahamiaji wa ndani wa JKK. Ijumatatu, ndege iliokodiwa na UM, iliochukua tani 36 ya mahitaji ya kufarajia umma huo, iliwasili Entebbe, Uganda.

WFP inapendekeza ifadhiliwe tani 55,000 za chakula, kuhudumia waathiriwa wa mapigano

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) linakadiria jumla ya watu waliong’olewa makazi katika eneo la mashariki, katika JKK, inapindukia milioni 1.3 (moja na laki tatu); na tani za chakula zinazohitajika kuwakidhia watu hawo mahitaji yao kuanzia kipindi cha sasa hadi mwishoni Aprili 2009 ni tani 55,000, ambao utaigharimu jumuiya ya kimataifa dola milioni 61. ~~

Huduma za kiutu zimezorotishwa JKK kutokana na mapigano

Elizabeth Byrs, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) Ijumaa aliwaelezea waandishi habari mjini Geneva juu ya vizuizi vinavyokwamisha sasa hivi zile huduma za kugawa misaada ya kiutu kwa umma muhitaji, kufuatia mapigano yaliofumka karibu na maeneo ya Goma na Grand Nord, ambapo hali inasemekana huko bado ni shwari.

Mashirika ya UM yahudumia misaada ya kihali kwa waathiriwa raia katika JKK

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) linaendelea kugawa posho ya chakula kwa wahamiaji wa ndani 135,000 katika kambi sita za muda, ziliopo Goma, mji wa mashariki katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

WFP inaendelea kugawa chakula Goma

Kwa mujibu wa Msemaji wa MONUC ndege ya shehena ya aina ya C130, iliofadhiliwa UM na Serikali ya Ubelgiji, hutua kila siku Goma na bidhaa za chakula za Shirika la WFP, shirika ambalo tangu Ijumatano limeanza kugawa posho ya chakula kwa wahamiaji wa ndani 135,000 waliopo katika zile kambi sita karibu na mji wa Goma.~~