Msaada wa Kibinadamu

UNICEF/WHO kufadhiliwa dola milioni 9.7 na Waqf wa Gates kuhudumia watoto dawa bora

Taarifa iliotolewa bia leo hii na mashirika mawili ya UM yanayohudumia maendeleo ya watoto, yaani UNICEF, na afya duniani, yaani WHO, imepongeza msaada wa dola milioni 9.7 waliopokea kutoka Waqf wa Bill na Melinda Gates, kwa makusudio ya kuimarisha utafiti wa kutengeneza dawa zitakazotumiwa makhsusi, na kwa urahisi, na watoto wadogo chini ya umri wa miaka kumi na tano.

Msemaji wa UNRWA akiri hali shwari Ghaza lakini bado ni ya wasiwasi

Chris Gunness, Msemaji wa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kihali kwa WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) alihojiwa Ijumatatu, kwa kupitia njia ya simu, na Idhaa ya Redio ya UM-Geneva ambapo alielezea namna hali ilivyo sasa hivi katika Ghaza, baada ya kutangazwa vikosi vya Israel vinasimamisha mashambulizi:~

Ofisa wa UNRWA anasema hali Ghaza ni ya kutisha mno

John Ging, Mkurugenzi wa Operesheni za Shirika la UM la Kufarajia Wahamiaji wa KiFalastina kwenye Mashariki ya Karibu (UNRWA) ameiambia Ofisi ya UM, Geneva, hii leo, kwa kutumia njia yasimu, ya kwamba mipangilio ya kuhudumia misaada ya kihali Ghaza, kwa umma muhitaji, imevurugwa kwa sasa, kwa sababu ya kuendelea kwa mapigano, hali ambayo vile vile alisema imeongeza khofu na wasiwasi miongoni mwa wakazi wa Ghaza pamoja na umma wa eneo jirani.

Haki za binadamu zakiukwa Ghaza, inasema UM

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu baada ya majadiliano ya siku mbili, kwenye kikao cha dharura, Ijumatatu mjini Geneva limepitisha azimio lenye kulaani vikali operesheni za kijeshi zinazoendelea sasa hivi za vikosi vya Israel kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Ghaza.

WFP kuanzisha operesheni za kuokoa maisha ya mamia elfu Ghaza

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha huduma ijulikanayo kama Operesheni za Kamba ya Kuokolea Ghaza, yenye lengo la kuhudumia watu wenye njaa ambao idadi yao inaendelea kuongezeka kila kukicha, tangu Israel kuanzisha mashambulio yake karibu wiki tatu zilizopita.

WFP yasihi mapigano yasitishwe ili itathminie mahitaji ya umma wa Ghaza

Hii leo, Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa mwito maalumu, kwa makundi yanayohasimiana katika eneo la Tarafa ya Ghaza, kusitisha mapigano na kuruhusu wahudumia misaada ya kiutu angalau kupata “upenu wa kupumua” utakaowawezesha kutathminia vyema mahitaji halisi ya umma waathirika katika Ghaza, ili baadaye kuwapatia wakazi hawo misaada ya kihali, ya kunusuru maisha.