Msaada wa Kibinadamu

UNHCR inasema nusu ya wahamiaji duniani huishi mijini

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba zaidi ya asilimia 50 ya wahamiaji milioni 10.5 wanaosaidiwa na taasisi hii ya kimataifa, huwa wanaishi kwenye maeneo ya miji na miji mikuu ya sehemu mbalimbali za dunia.

Ripoti ya IFRC inasihi, huduma za misaada ya kihali Afrika zahitajia marekibisho ya hali ya juu

Ripoti mpya ya Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC), iliochapishwa hii leo, imeonya kwamba misaada ya kiutu inayofadhiliwa bara la Afrika ni ya gharama kubwa, na mara nyingi inashindwa kukidhia mahitaji yanayoendelea kupanuka, kwa zile jamii dhaifu kihali, ziliopo katika sehemu mbalimbali za Afrika.

IOM imetangaza kuwapatia IDPs wa Zimbabwe hifadhi na misaada ya dharura

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuanzisha mradi mpya wa kuwasaidia kidharura wahamiaji wa ndani (IDPs) waliong\'olewa makazi katika Zimbabwe kupata hifadhi wanayohitajia kumudu maisha.

Mashirika ya UM yanahudumia kihali WaAngola waliofukuzwa kutoka JKK

Ofisi ya OCHA imeripoti raia wa Angola waliofukuzwa JKK na waliorejea nchini mwao hivi sasa wanajumlisha watu 51,000.

Uspeni imeongeza maradufu mchango wake kwa WFP kupambana na njaa katika Pembe ya Afrika

Soraya Rodriguez Ramos, Waziri wa Nchi wa Uspeni kwa Ushirikiano wa Kimataifa, ametangaza siku ya leo kuwa serikali yao imekabidhi Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) msaada wa Yuro milioni 75 (dola milioni 112) kutumiwa kufarajia hali mbaya ya chakula iliolivaa eneo la Pembe ya Afrika.

UM yahimiza Mataifa Wanachama yote kushirikiana kufyeka njaa duniani

Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), kwenye risala aliotoa mnamo siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula unaofanyika Roma, Utaliana, alisema raia wote wa kimataifa - na sio viongozi wa dunia pekee - wanawajibika kuhamasishwa wajitayarishe kuwapatia chakula watu bilioni moja ziada wenye kusumbuliwa na tatizo la njaa sugu ulimwenguni.

Mchanganyiko wa vitega uchumi na nia ya kisiasa huweza kufyeka njaa - FAO

Ripoti mpya ya Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), iliochapishwa rasmi leo hii, yenye kutathminia maendeleo yaliofanyika kwenye nchi kadha inazozishughulikia, imebainisha kwamba idadi ya watu wasiopata chakula cha kutosha iliteremka kwa kiwango kikubwa, na cha kutia moyo.

OCHA inasihi, misaada ya dharura yahitajika kuunusuru umma wa Usomali na majanga ya kiutu

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeihimiza jumuiya ya kimataifa, kuharakisha michango ya dharura inayotakikana kunusuru maisha kwa raia wa Usomali.

Nchi maskini 31 zimedhurika na bei ya juu ya chakula: FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwamba ulimwengu unakabiliwa na uhaba mkubwa, na wa hatari wa chakula, ulioathiri vibaya sana nchi 31.