Msaada wa Kibinadamu

Wakulima wadogo wadogo wa Tanzania kupatiwa na FAO misaada ya kukuza kilimo na taaluma ya masoko

Shirika la UM kuhusu Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti juu ya mradi utakaotumiwa kuimarisha kilimo katika Tanzania, unaokusudiwa kuwasaidia wakulima kuongeza uwezo wa kufikia masoko na kuuza bidhaa zao, hali ambayo itakuza akiba ya chakula nchini.

FAO imechapisha mwongozo mpya kusaidia utetezi wa haki ya kupata chakula

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limechapisha taarifa inayojulikana kama "taarifa ya utaratibu wa sanduku la vifaa" juu ya haki ya kupata chakula, mfumo ambao umekusudiwa kuzipatia nchi wanachama, taasisi za kimataifa, jumuiya za kiraia na wadau wengineo hati zinazofaa kutumiwa kutetea haki ya kupata chakula, haki ambayo ni sawa na haki za kimsingi za wanadamu.

UM kuhadharisha, watu milioni sita ziada Ethiopia wanahitajia misaada ya chakula kuwavua na janga la njaa

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti Ethiopia imezongwa na mshtuko mkuu wa maafa yenye kuathiri hali ya chakula kwa watu milioni 6 nchini.

Waathirika milioni sita ziada wa ukame Ethiopia wanahitajia misaada ya dharura ya chakula

Serikali ya Ethiopia na mashirika ya kimataifa yenye kuhusika na misaada ya kiutu yametangaza kunahitajika mchango wa dharura ziada wa dola miilioni 175 kwa mwaka huu, kuhudumia kihali watu milioni 6.2 walioathirika sana na mavuno haba na ukame wa muda mrefu uliosakama katika Ethiopia katika kipindi cha karibuni.

Ofisa wa UNICEF anasema watoto wamedhurika zaidi na athari za mgogoro sugu wa JAK

Hilde Johnson, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), baada ya kuzuru Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK) ameeleza kwamba matatizo yaliolizonga taifa hilo huathiri pakubwa watoto wadogo, na hali hiihuenda ikaharibika zaidi pindi wahisani wa kimataifa watashindwa kuharakisha misaada inayohitajika kidharura kuhudumia kihali watoto hawa.

Huduma za ndege za UM, za kugawa misaada ya kiutu Ethiopia, zahatarishwa kusitishwa

Jumuiya ya Kundi Linalotumia Huduma za Usafiri wa Ndege za Kugawa Misaada ya Kiutu, ambalo hujulikana kama Kundi la UNHAS, imetangaza leo kwamba italazimika kusitisha operesheni zake nchini Ethiopia - hasa kwenye lile Jimbo la raia Wasomali - kwa sababu ya upungufu wa fedha kutoka wahisani wa kimataifa.

OCHA inasema haki za binadamu zinaendelea kuharamishwa na makundi yanayohasimiana katika JKK

Elizabeth Byrs, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) leo aliwaambia waandishi habari mjini Geneva kwamba taasisi yao inalaani ukiukaji wa haki za binadamu, unaoendelezwa na makundi yanayohasmiana katika JKK.

Watu 160,000 katika JKK watafaidika na msaada wa chakula wa WFP uliovuka kilomita 1,000

Msafara wa malori 13 yaliobeba chakula, yanayomilikiwa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) yamewasili kwenye mji wa Dungu wiki hii, eneo la kaskazini-mashariki katika JKK, baada ya safari ya kilomita 1,000 ambayo ilianzia Uganda, na kupitia Sudan Kusini, hadi Kongo.

Mataifa ya Bahari ya Hindi kushiriki kwenye mazoezi ya tahadhari za mapema dhidi ya dhoruba za tsunami

UM umetangaza kwamba mnamo tarehe 14 Oktoba, nchi 18 ziliopo kwenye eneo linalojulikana kama Mzingo wa Bahari ya Hindi zitashiriki kwenye mazoezi ya tahadhari kinga dhidi ya ajali ya mawimbi ya tsunami.

BU lasisitiza wanawake washirikishwe kikamilifu katika ujenzi wa amani

Baraza la Usalama (BU) leo limefanyisha mkutano wa hadhara, wa siku nzima, ambao wawakilishi wa kimataifa 55 walizungumzia kuhusu suala la ‘Wanawake, Amani na Usalama\'.