Msaada wa Kibinadamu

Kituo cha kuwasaidia wahamiaji jirani kupata ajira chafunguliwa mpakani Afrika Kusini: IOM

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limetangaza kufunguliwa Kituo cha Wahamaji wa Ajira katika Afrika Kusini, kwenye mji wa mipakani wa Beitbridge.

Ofisa wa UNHCR anasailia mzozo wa makazi kwenye kambi za wahamiaji za Dadaab, Kenya

Katika miezi ya karibuni, vurugu na mizozo ya kihali ilikithiri kwa wingi katika Usomali, hali iliosababaisha maelfu ya raia kuamua kuhama makwao na kuelekea mataifa jirani kutafuta hifadhi na usalama.

Msaada wa dola 500,000 wafadhiliwa na UNICEF kuhudumia miradi ya kijamii Kongo-Brazzaville

Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) ametangaza wakati anazuru Jamhuri ya Kongo (Brazzavile) wiki hii ya kuwa watafadhilia msaada wa dola 500,000 ili kuhudumia miradi ya lishe bora, afya na ilimu nchini humo, sekta ambazo ziliathiriwa zaidi na mizozo ya uchumi wa dunia na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wale raia walio dhaifu kihali.

WFP imeomba dola milion 230 kuhudumia dharura ya chakula Kenya

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa ombi la kutaka lifadhiliwe na wahisani wa kimataifa, msaada wa dola milioni 230 kuhudumia dharura ya chakula kwa Kenya katika kipindi cha miezi sita ijayo.

WFP imeamua kudondosha kutoka angani chakula kwa wakazi muhitaji wa JKK

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limearifu kwamba litaandeleza operesheni za kuwapatia chakula raia 10,000 muhitaji waliopo katika eneo la Dingile, katika mashariki ya JKK kwa kuidondosha misaada hiyo kutoka kwenye ndege.

WFP inasema hali ya chakula Darfur inatia wasiwasi

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), ambalo linahudumia misaada ya kihali kwa watu milioni 3.6 katika Jimbo la Magharibi la Sudan la Darfur limeripoti kukabiliwa na majukumu ziada baada ya mashirika wenzi, yasio ya kiserikali, kufukuzwa Sudan mnamo mwanzo wa mwaka huu.

UM umepokea chini ya nusu ya maombi ya msaada unaohitajika Zimbabwe

Mratibu wa misaada ya kiutu ya UM katika Zimbabwe, Augustino Zacarias ametoa taarifa iliotahadharisha kwamba "ijapokuwa Zimbabwe haikabiliwi na mapigano au vurugu, hata hivyo matishio ya kihali, mathalan, upungufu wa chakula, miripuko ya maradhi ya kuambukiza kama kipindupindu, ni matatizo ambayo bado yanaendelea kusumbua taifa."

UNHCR kuhamisha tena wahamiaji wa Dadaab, Kenya

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliripoti leo kutoka Geneva kwamba taasisi yao imeanzisha rasmi, wiki hii, operesheni za kuwahamisha wahamiaji wa Usomali 12,900 kutoka kambi ya Dadaab, iliosongamana watu kupita kiasi, na kuwapeleka wahamiaji kwenye kambi ya makaazi ya muda ya Kakuma, iliopo kaskazini-magharibi nchini Kenya.

Huduma ndege za WFP katika Chad zafadhiliwa dola milioni moja

Imetangazawa kutoka Geneva ya kwamba Ndege za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) zitafadhiliwa msaada wa dola milioni moja kutoka Serikali ya Marekani, utakaotumiwa kuhudumia misaada ya kiutu katika Chad kwa mwezi mmoja ziada. Mnamo siku za karibuni, WFP ilikabiliwa na tatizo la kusitisha huduma hizo kwa sababu ya upungufu wa fedha.

UNICEF imeripoti hali ya usalama itachelewesha ugawaji wa misaada ya kunusuru maisha Usomali

Taarifa ilitoka Nairobi siku ya leo ya Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) imeeleza kuwa shirika litaakhirisha kupeleka misaada ya chakula cha kunusuru maisha ya watoto 85,000, wanaoteseka na utapiamlo hatari, katika baadhi ya sehemu za majimbo ya Usomali ya kati na kusini, kwa sababu ya kukithiri kwa uhasama dhidi ya watumishi wa mashirika yanayohudumia misaada ya kihali.