Msaada wa Kibinadamu

Viongozi wa G-8 wameahidi msaada wa kilimo wa $20 bilioni kwa nchi masikini

Viongozi wa Kundi la G-8 waliokutana kwenye mji wa L\'Aquila, Utaliana kabla ya kuhitimisha kikao chao waliahidi kuchangisha dola bilioni 20 za kuzisaidia nchi masikini kuhudumia kilimo, ili waweze kujitegemee chakula kitaifa badala ya kutegemea misaada ya kutoka nchi za kigeni, hali ambayo ikidumishwa itasaidia kukomesha duru la umaskini na hali duni.

Watu milioni 2.3 wenye VVU wafaidika na msaada wa 'Global Fund' wa dawa ya kurefusha maisha

Taasisi ya Mfuko wa Kimataifa Dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria – inayoungwa mkono na UM – yaani Taasisi ya Global Fund, imetangaza leo watu milioni 2.3 walioambukizwa na virusi vya UKIMWI ulimwenguni walifanikiwa kupatiwa ile dawa ya kurefusha maisha ya ARV, kutokana na miradi inayosimamiwa na Taasisi ya Global Fund. Muongezeko huu unawakilisha asilimia 31 ya watu waliohudumiwa tiba hiyo, tukilinganisha na takwimu za mwaka jana.

UNHCR yafadhilia utafiti wa athari za KiIslam kwenye sheria ya hifadhi ya wahamiaji

Profesa Ahmed Abu al-Wafa, mtaalamu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Cairo, ameandika kitabu chenye jina lisemalo "Utafiti wa Kulinganisha: Haki ya Kupata Hifadhi na Usalama Baina ya Shari\'ah ya KiIslam na Sheria ya Kimataifa ya Wahamiaji".

Wahisani wahimizwa na UNCTAD kutekeleza ahadi za kuimarisha kilimo Afrika

Kwenye kikao cha Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kilichofanyika Ijumanne Geneva kuzingatia mzozo wa chakula katika Afrika, wahisani wa kimataifa walihimizwa kutekeleza haraka ahadi walizotoa siku za nyuma kuimarisha kilimo bora barani humo.