Msaada wa Kibinadamu

OCHA imeripoti 170,000 wahajiri Mogadishu kufuatia mfumko mpya wa mapigano

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mapigano yalifumka tena katika wilaya za Mogadishu za Karaan na Hodan mnamo mwisho wa wiki iliopita.

Hifadhi bora kwa raia walionaswa kwenye mapigano inazingatiwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limefanyisha kikao cha hadhara Ijumaa kuzingatia ulinzi wa raia kwenye mazingira ya mapigano na vurugu.

Mfuko wa CERF kuifadhilia IOM msaada wa kuhudumia makazi ya muda wahamiaji wa Usomali

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti kuwa litapokea msaada wa dola milioni 2.6 kutoka Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF, fedha zitakazotumiwa kuwasaidia kupata makazi ya dharura wahamiaji 12,700 wa Usomali ambao wanabanana hivi sasa kwenye kambi za Kakuma, ziliopo Dadaab, kwenye jimbo la kaskazini-mashariki ya Kenya.

Mkutano wa kudhibiti athari za maafa wapendekeza vifo vipunguzwe kwa nusu 2015

Mkutano wa Kimataifa Kupunguza Hatari Inayoletwa na Maafa umemalizika mjini Geneva leo Ijumaa, ambapo kulitolewa mwito maalumu unaowataka viongozi wa kisiasa katika Mataifa Wanachama kuchukua hatua za dharura kupunguza, angalaukwa nusu idadi ya vifo vinavyosababishwa na maafa ya kimaumbile itakapofika 2015, .

Wanariadha wa kimataifa kushiriki kwenye miradi ya kupiga vita njaa ulimwenguni

Jarno Trulli na Timo Glock, madereva wa mashindano ya mbio za gari, wenye kuwakilisha kampuni za Panasonic na Toyota, wanatazamiwa kuvalisha na kupamba gari zao na alama ya kitambulisho ya lile Shirika UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), pale watakaposhiriki kwenye mashindano ya gari Uingereza mnamo Ijumapili ijayo.

WFP inahadharisha, Pembe ya Afrika inakabiliwa tena na mwaka wa njaa

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa onyo maalumu leo hii kutoka ofisi zake ziliopo Roma, Italiana, linalohadharisha kwamba mamilioni ya watu wanaoishi katika Pembe ya Afrika wanakabiliwa, kwa mara nyengine tena, na mchanganyiko maututi wa ukame ulioselelea, mvua haba na mizozo isiokwisha, katika mazingira ambayo bei ya chakula, hususan kwenye nchi nyingi zinazoendelea, nayo pia bado inaendelea kuwa ya juu kabisa.

Walimwengu waandamana kuunga mkono juhudi za WFP kupiga vita njaa duniani

Ijumapili ya tarehe 07 Juni (2009) makumi elfu ya watu, katika sehemu mbalimbali za dunia, walikusanyika kwenye miji kadha ya kimataifa, na kuandamana kuunga mkono juhudi za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) katika kupiga vita tatizo la njaa ulimwenguni, hususan miongoni mwa watoto wadogo.

FAO yatoa mwito wa kubuniwa mfumo imara dhidi ya njaa

Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) ametoa mwito maalumu, uitakayo jamii ya kimataifa kuimarisha mfumo wa utawala bora wa kukabiliana na matatizo ya njaa, kwa kuhakikisha akiba ya chakula katika ulimwengu itadhaminiwa kwa taratibu zitakoridhisha na kutimiza mahitaji ya chakula ya muda mrefu kwa umma wa kimataifa.

Zimbabwe itahitajia dola milioni 719 kuhudumia kidharura umma

UM imeripoti Zimbabwe inahitajia wahisani wa kimataifa kuchangisha msaada wa dharura, kwa mwaka huu, unaokadiriwa dola milioni 719 kukidhi mahitaji ya kiutu kwa umma na kufufua uchumi nchini, baada ya shughuli hizo kuporomoka nchini karibu miaka kumi.