Msaada wa Kibinadamu

Bei kuu ya chakula katika nchi masikini inaendelea kutesa mamilioni, kuhadharisha FAO

Kwenye ripoti iliotolewa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) - yenye mada isemayo ‘Hali ya Chakula na Matarajiao ya Baadaye ya Mavuno\' - ilieleza kwamba bei ya juu ya chakula katika mataifa yanayoendelea inaendelea bado kusumbua na kuwatesa mamilioni ya umma masikini, raia ambao tangu mwanzo umeathirika na matatizo sugu ya njaa na utapiamlo, licha ya kuwa mavuno ya nafaka ulimwenguni, kwa ujumla, yameongezeka katika kipindi cha karibuni, na bei za chakula ziliteremka kimataifa, hali kadhalika.

Utatuzi Mbadala wa Mzozo wa Chakula Duniani

Mnamo wiki hii, David Nabarro, aliyeteuliwa kuongoza Tume ya UM juu ya Mzozo wa Chakula Duniani amehadharisha kwamba licha ya kuwa,katika siku za karibuni bei za chakula duniani ziliteremka kwa kiwango kikubwa sana, tukio hilo halikufanikiwa kuuvua umma wa nchi masikini na tatizo la njaa. Mamilioni ya watu duniani bado hawana uwezo wa kupata chakula kwa sababu ya mchanganyiko wa ufukara na mporomoko, usio wa kawaida, wa shughuli za uchumi, kijumla.

Wahudumia misaada ya kiutu Darfur watekwa nyara

Wafanyakazi wa kike wawili wenye kuhudumia misaada ya kihali Darfur Kusini, wanaowakilisha mashirika yasio ya kiserikali ya Ufaransa, Ijumapili usiku, walitekwa nyara kutoka makazi yao baada ya kushikiwa bunduki wao na walinzi, na majambazi wasiotambulika.

Mijadala leo katika Makao Makuu

Baraza la Udhamini leo linazingatia suala la mgogoro wa chakula duniani, na pia kujadilia sera za kutumiwa, kipamoja, na Mataifa Wanachama ili kuhakikisha haki ya mwanadamu kupata chakula hutekelezewa umma wa kimataifa kote ulimwenguni.

UM kuchangisha msaada wa kuihudumia Namibia kudhibiti athari za mafuriko

UM unajishughulisha hivi sasa kuchangisha dola milioni 2.7 zinazohitajika kuisaidia Jamhuri ya Namibia kudhibiti bora athari za mafuriko nchini, yaliosababishwa na mvua kali za karibuni ambazo zilin\'goa makazi watu 13,000 na pia kuharibu majumba na njia za kujipatia rizki kwa jumla ya watu 350,000.