Msaada wa Kibinadamu

Taarifa ziada za huduma za kihali za UM katika Goma

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetupatia taarifa mpya kuhusu juhudi za UM katika ugawaji wa misaada ya kihali katika Goma na maeneo jirani, hususan kwa wale wahamiaji muhitaji walioathirika na mapigano yaliozuka karibuni baina ya vikosi vya Serikali na makundi ya waasi wa CNDP.

Mwanajeshi wa UNAMID ameuawa Darfur

UM umeripoti kwamba askari mmoja wa Afrika Kusini ameuawa na mwengine amejeruhiwa vibaya kutokana na shambulio liliofanyika kilomita 3 kutoka kambi yao iliopo Kutum, Darfur kaskazini.

Hali ya wahamiaji katika JKK inasailiwa na UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba ofisi zake ziliopo Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) sasa zinajiandaa kuhudumia misaada ya kihali kwa makumi elfu ya watu waliolazimika kuhajiri vijiji na kambi za wahamiaji wa ndani, kwa sababu ya kuzuka mapigano baina ya waasi na vikosi vya serikali katika eneo la kaskazini.

UM kuifadhilia Yemen misaada ya kihali kwa waathiriwa wa mafuriko

Kadhalika UNHCR imeripoti kuingiwa na wasiwasi kuhusu hali ya raia 10,000 wa Yemen wanaohitajia kufadhiliwa misaada ya kihali, haraka iwezekanavyo, kutoka mashirika ya UM na yale yasio ya kiserikali, baada ya gharika iliyowakumba kufuatia mafuriko yaliozushwa na mvua kali iliopiga kwenye majimbo ya Hadhramout, Al Mahra na sehemu nyengine nchini zilizotangazwa na Serikali ya kuwa ni maeneo ya maafa.

Cuba itasaidiwa na WFP kuhudumia waathiriwa wa vimbunga Gustav na Ike

Halkadhalika, Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) linajiandaa pia kutuma misaada ya kihali ya kuwavua na maafa ya kimaumbile watu milioni 1.78 katika Cuba, umma ambao uliathiriwa sana na vimbunga vya Gustav na Ike, vilivyopiga taifa hilo katika mwisho wa mwezi Agosti na mwanzo wa Septemba.

WFP itafadhilia watoto Usomali msaada wa chakula dhidi ya utapiamlo

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) linatarajiwa karibuni kuanza kupeleka misaada ya chakula cha dharura chenye rutubishi kubwa katika Usomali, aina ya biskuti zilizotengenezewa njugu na karanga, ikiwa miongoni mwa juhudi za kuwakinga watoto na hatari inayoendelea kukithiri ya utapiamlo mbaya uliozuka nchini humo uliopaliliwa zaidi na mapigano.

UM una wasiwasi juu ya marekibisho ya haki ya kupata hifadhi kwa wahamiaji Yemen

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamaiji (UNHCR) limeiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemen iipatie UM fafanuzi halisi kuhusu tangazo lenye kudai wahamiaji wa kutoka Ethiopia na Eritrea hawatoruhusiwa tena kuingia nchini.

Mafuriko Kenya yahitajia misaada ya kimataifa, inasema OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba nchini Kenya, katika wilaya ya Mandera, mvua kali zilizonyesha huko karibuni zilisababisha ukingo wa mto kubomoka na kuzusha mafuriko yalioathiri zaidi ya kaya 1,000.

UNHCR inakadiria takwimu za waomba hifadhi kwenye mataifa yalioendelea

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limechapisha ripoti mpya juu ya takwimu za wahamiaji wenye kuomba hifadhi ya kisiasa kwenye nchi zenye maendeleo ya kiufundi, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

UNHCR imefichua mapengo kwenye huduma za kimsingi kwa wahamiaji duniani

L. Craig Johnstone, Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Alkhamisi aliwasilisha ripoti yenye kuonyesha kuwepo pengo kubwa katika utekelezaji wa ule mradi wa majaribio ya kukidhia mahitaji halisi ya wahamiaji katika mataifa manane yanayohudumiwa na UNHCR – ikijumlisha Cameroon, Ecuador, Georgia, Rwanda, Thailand, Tanzania, Yemen and Zambia.