Msaada wa Kibinadamu

Mafuriko Afrika Magharibi yahatarisha afya ya umma

Mataifa ya Benin, Burkina Faso, Niger, Mali na pia Mauritania na Togo yamekabiliwa, sasa hivi, na maafa ya mvua kali zinazobashiriwa kuendelea hadi mwezi Septemba na kuhatarisha afya za mamilioni ya watu wanaoishi kwenye maeno haya ya Afrika Magharibi.

Uholanzi imebuni maabara maalumu itembeayo kuisaidia UNEP kukabili maafa

Serikali ya Uholanzi imewasilisha aina ya maabara maalumu ya magari iliobuniwa kutumiwa kukabiliana na dharura za kimazingira kimataifa. Mabara ya aina hii itatumiwa kulisaidia Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) kupata uwezo wa kusafiri, kwa haraka, kwenye maafa ya dharura ya kimazingira ili kupima, kwa utaalamu unaoaminika, hali kwa kuhusiana na vitu vya sumu vinavyohatarisha maisha. Maabara hii itajulikana kama Maabara ya Kutathminia Hali ya Mazingira (EAM) na itakuwa inapelekwa kwenye mataifa yanayoendelea yaliokosa utaalamu na uwezo unaohitajika kudhibiti kidharura maafa ya kimazingira.~

Hifadhi ya muda ya wageni wakaazi huenda ikasitishwa Afrika Kusini

Ripoti ya awali wiki hii itasailia hali ya wageni Afrika Kusini, ambao mnamo miezi miwili iliopita waliathirika na vurugu liliofumka nchini humo dhidi yao. Tutalenga ripoti juu ya hifadhi ya muda ya makazi kwa wahamiaji hawo katika jimbo la Gauteng.~

Waathiriwa wa mapigano Georgia kupatiwa msaada wa chakula na WFP

Ndege mbili za aina ya Antonov 12 zilizokodiwa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo asubuhi zilianza safari ya kuelekea Georgia kutokea mji wa Brandisi, Utaliana zikibeba shehena ya tani za metriki 34 za biskuti maalumu za chakula zitakazogaiwa maelfu ya watu waliongo’lewa makwao ambao walidhurika kihali na mapigano yalioshtadi karibuni kwenye eneo lao.

Ripoti fupi kuhusu mzozo wa Ossetia Kusini

Hali ya eneo la machafuko na vurugu katika jimbo liliojitenga la Georgia, katika Ossetia Kusini, inaendelea kuwa ya vurugu na utumiaji nguvu, na UM haukufanikiwa kuhudumia kihali umma raia waathiriwa wa mzozo huo kama inavyopaswa.~~ Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kunahitajika kufunguliwa ushoroba mpya wa usalama utakaotumiwa na magari ya mashirika ya kimataifa kupeleka misaada ya kiutu kwenye eneo la mapigano.

Kanada kutuma manowari Usomali kulinda meli za chakula za WFP

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kukaribisha uamuzi wa serikali ya Kanada wa kupeleka manowari kwenye mwambao wa Usomali, itakayotumiwa kusaidia kulinda zile meli zinazochukua shehena ya chakula inayopelekwa umma wa Usomali kunusuru maisha. Meli hizo huwa zinakodiwa na WFP na mara nyingi hutekwa nyara na maharamia wanaovizia kwenye mwambao wa Afrika Mashariki katika Bahari ya Hindi.

Wafalastina walionyimwa makazi Iraq kuhamishiwa Iceland na Sweden

Wafalastina zaidi ya darzeni mbili walio hali dhaifu na waliokwama kwa muda wa miaka miwili kwenye kambi ya wahamiaji ya Al Waleed, iliopo jangwani kwenye mipaka kati ya Iraq na Syria, wanatarajiwa kuhamishiwa Iceland katika wiki mbili zijazo.