Msaada wa Kibinadamu

Utaalamu na mahema kufadhiliwa Afrika Kusini na UNHCR kwa waathiriwa wa hujuma za chuki

Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Geneva, Ron Redmond alipokutana na waandishi habari wa kimataifa Ijumaa aliripoti ya kuwa taasisi yao imepeleka misaada ya dharura Afrika Kusini itakayochangia juhudi za Serikali katika kuwahudumia kihali maelfu ya waathiriwa wageni waliong\'olewa makwao baada ya kushambuliwa kibaguzi karibuni nchini humo.~

Askofu Mkuu wa Afrika Kusini aomba vikwazo Ghaza vikomeshwe

Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu ameiambia Redio ya UM ya Geneva kwamba alishtushwa sana kwa aliyoyaona kuhusu maisha duni ya umma wa Wafalastina waliopo eneo liliokaliwa kimabavu la Tarafa ya Ghaza, ambalo analizuru hivi sasa.

Juhudi za UM kuishawishi Myanmar kupokea misaada ya kiutu ya kimataifa

Ijumapili mataifa zaidi ya 50, yalihudhuria kikao maalumu mjini Yangon, Myanmar, kilichotayarsihwa kidharura na Wanachama wa Umoja wa Mataifa ya Kusini ya Asia (ASEAN) kwa makusudio ya kuchangisha fedha za kusaidia kihali fungu kubwa la umma wa Myanmar uliodhuriwa na Kimbunga Nargis kilichopiga huko tarehe pili Mei.

Huduma za mashirika ya UM katika Myanmar zasonga mbele

Elizabeth Byrs, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) ameripoti kutoka Geneva kwamba hivi sasa juhudi za ugawaji wa misaada ya kiutu kwa waathiriwa wa Kimbunga Nargis zimefanikiwa kuwafikia watu milioni moja katika Myanmar, wingi wao wakiwa wakaazi wa mji mkuu wa Yangon. Kadhalika, aliripoti ya kuwa watu 470,000 nao pia walipatiwa huduma za dharura na mashirika ya kimataifa, ikiwa miongoni mwa watu milioni 2 muhitaji wanaoishi kwenye miji 15 iliopata madhara makubwa ya Kimbunga Nargis.

Mtaalamu wa UM anahimiza juhudi ziongezwe kusaidia IDPs Kenya

Hivi karibuni, Walter Kaelin, Mjumbe wa KM juu ya Wahamiaji wa Ndani Waliong’olewa Makwao, au Wahamiaji wa IDPs, alizuru Kenya kwa siku nne kutathminia hali ya wale watu waliohamishwa makazi kwa nguvu kutokana na vurugu liliozuka nchini kufuatilia uchaguzi wa taifa mnamo mwisho wa 2007.

IOM/UNICEF yashirikiana kuhudumia waathiriwa wa mashambulio ya chuki za wageni Afrika Kusini

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limeripoti kwamba linashirikiana na UNICEF kuwasaidia waathiriwa wa mashambulio ya chuki za wageni Afrika Kusini kurejea makwao. Msemaji wa IOM Geneva, Jemini Pandya alitupatia fafanuzi zake kuhusu suala hili.

Waliong'olewa mastakimu Sudan kusini wahitaji kusaidiwa kimataifa kunusuru maisha, OCHA imenasihi

Msemaji wa Ofisi ya OCHA, Elizabeth Byrs ameripoti kwamba wakaazi wa mji wa Abyei, Sudan waliokimbilia kusini baada ya kuzuka mapigano kati ya vikosi vya Serikali na kundi la SPLM, nao vile vile wanahitajia kusaidiwa kihali na jumuiya ya kimataifa kabla hali yao ya maisha haijaharibika zaidi.

Wahudumia misaada ya kiutu waruhusiwa kuingia Myanmar baada KM kuonana na Kiongozi wa Taifa

KM Ban Ki-moon Ijumaa alikutana na kiongozi wa Myanmar, Jenerali Mkuu Than Shwe kwenye mji mkuu wa Naypidaw ambako waliendeleza mazungumzo ya saa mbili yaliozingatia taratibu za kuridhisha, zitakazosaidia kipamoja kuharakisha ugawaji wa misaada ya kiutu kwa umma ulioathirika na uharibifu wa Kimbunga Nargis, ambacho kiligharikisha Myanmar, wiki tatu iliopita.

UNHCR kuhudumia waathiriwa wa hujuma za wageni Afrika Kusini

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR)limeripoti kushiriki kwenye juhudi za kuhudumia misaada ya kihali wale wahamiaji walioathirika karibuni na mashambulio ya chuki za wageni, yaliotukia katika jimbo la Gauteng, kaskazini mashariki katika Afrika Kusini.

KM azuru maeneo yaliogharikishwa na tufani Myanmar

KM Ban Ki-moon amewasili Myanmar Alkhamisi ambapo alikutana, kwa mashauriano na Waziri Mkuu, Jenerali Thein Sein na pia mawaziri wengineo ambao walisailia taratibu za kuchukuliwa kipamoja katika kuharakisha ugawaji wa misaada ya kihali kwa umma waliodhurika na janga la Kimbunga Nargis liliolivaa taifa hilo wiki tatu nyuma. Alasiri KM alipata fursa ya kuzuru eneo la Delta la Irrawaddy, na kujionea mwenyewe binafsi athari za uharibifu wa Kimbunga Nargis kieneo.