Msaada wa Kibinadamu

Maelfu ya raia CAR wakimbilia vichakani na kunyimwa mahitaji ya kimsingi

Toby Lanzer, Mshauri wa Umoja wa Mataifa juu ya Misaada ya Dharura kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwenye mkutano na waandishi habari katika Makao Makuu ya UM alibainisha kwamba mashirika ya UM yanakabiliwa na tatizo gumu la kuhudumia misaada ya kiutu fungu kubwa la wahamiaji wa ndani ya nchi 200,000 waliokimbilia vichakani kaskazini katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Wahamiaji hawa huwa wanakimbilia vichakani kuwakwepa majambazi wenye silaha ambao hushambulia raia kihorera.

WFP imeanza kugawa chakula Bukini kwa waathiriwa wa Tufani Ivan

Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha huduma za dharura za kugawa chakula katika yale maeneo ya Bukini yaliodhirika na uharibifu wa Tufani Ivan iliopiga wiki iliopita. Makumi elfu ya watu wanategemea misaada hiyo ya kihali kutoka mashirika ya UM, hususan ule umma unaoishi kwenye mahema mjini Antananarivo, ambao nyumba zao ziliharibiwa na tufani, pamoja na wale watu wanaoishi kwenye sehemu za mwambao wa mashariki ya Bukini na kwenye kisiwa cha St. Marie, maeneo yalioumia zaidi na gharika ya Tufani Ivan.

UNICEF yajitolea kufufua elimu ya msingi Liberia

Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF), ambaye anazuru Liberia wiki hii, ametangaza kufadhilia taifa hilo msaada wa dola milioni 20 zitakazotumiwa kufufua tena sekta ya ilmu ya msingi, ambayo iliharibiwa na vile vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshtadi nchini humo kwa muda wa miaka kumi na tano.

El Geneina kupokea Wadarfuri waliokosa makazi

UNHCR imeripoti ya kuwa karibuni kumefunguliwa kambi mpya nje ya El Geneina, Darfur Magharibi zilizoandaliwa kupokea wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) 6,000 waliohajiri makwao baada ya uhasama kufumka tena kwenye eneo lao.

Eritrea imekakamaa kuiwekea UNMEE vikwazo

Shirika la Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia/Eritrea (UNMEE) limearifu kwamba wanajeshi wa Eritrea bado wanaendelea kuwaekea vikwazo dhidi ya shughuli zake. UNMEE ilitoa mfano wa kitendo kilichotukia juzi ambapo magari 8 ya UM yalizuiliwa kuelekea mji wa Asmara kukusanya vifaa vya uhamisho wa muda vya watumishi wa UNMEE waliotarajiwa kupelekwa taifa jirani la Ethiopia.

UNHCR imesafirisha Kenya misaada ziada ya kiutu

Mnamo mwisho wa wiki iliopita, Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) lilipeleka nchini Kenya mahema 2,345 yatakayotumiwa na makumi elfu ya zile familia zilizong’olewa makwao baada ya machafuko kufumka nchini mwanzo wa mwaka kufuatia uchaguzi.

Walinzi Amani wa UNMEE wazuiliwa na Eritrea kwenda Ethiopia

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia na Eritrea (UNMEE) limeripoti kwamba wenye madaraka katika Eritrea bado wanaendelea kuzuia wanajeshi pamoja wafanyakazi wa kiraia wa UNMEE kuvuka mpaka kwenda uhamishoni wa muda nchini Ethiopia.

FAO itakithirisha misaada kwa waathiriwa wa mafuriko Kusini mwa Afrika

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limejiandaa kuongeza huduma zake kwa watu muhitaji milioni moja wanaoishi katika Malawi, Msumbiji, Zambia na Zimbabwe ambao waliathiriwa na uharibifu uliotifuliwa karibuni na mvua kali zilizozusha mafuriko yaliogharikisha mavuno na makazi. Kadhalika wapimaji wahali ya hewa wanaashiria mvua hizo zitaselelea kieneo hadi mwisho wa Machi, na wanakhofia zitauchochea Mto Zambezi kufura na kukuza uharibifu ziada kwenye maeneo husika ya kusini mwa Afrika.

UM utaisaidia Bukini kukabiliana vyema na athari za matofani

UM hivi sasa unaisadia Bukini kukabiliana na hasara kuu iliozushwa na Tufani Ivan ambayo mapema wiki hii ilipiga mwambao wa mashariki-kaskazini ya taifa hilo la Bahari ya Hindi. Bukini, ikisaidiwa na mashirika ya UM sasa wanaandaa kipamoja huduma za dharura za kuukinga umma na kimbunga kingine chenye jina la Tufani Hondo, ambayo tumearifiwa ipo njiani ikielekea eneo la mashariki.

UM wazuiliwa kuhudumia wahajiri wa Darfur walioingia Chad mashariki

Mnamo wiki iliopita wahajiri 8,000 ziada wa kutoka jimbo la Darfur Magharibi linalopakana na taifa jirani la Chad, walivuka mpaka kunusuru maisha baada ya kutukia mashambulio ya ndege kwenye maeneo yao.