Msaada wa Kibinadamu

Mtumishi wa WFP kuuawa baada ya mashambulio ya kuvizia Sudan ya kusini

Emmanuel Chaku Joseph, mwenye umri wa miaka 28, raia wa Sudan aliyeajiriwa udereva na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) aliuawa kikatili mnamo kati ya wiki baada ya kuzingiwa na kushambuliwa kwenye barabara kati ya Juba, mji mkuu wa Sudan kusini na mji wa Torit.

WFP kuhudumia chakula watu milioni 2 Sudan ya kusini kwa 2007

Shirika la WFP limeripoti kwamba litashiriki kwenye mpango wa kimataifa wa kuwahudumia chakula watu milioni 2 muhitaji waliopo Sudan ya kusini katika mwaka 2007.

Juhudi za UM kusuluhisha matatizo ya Pembe ya Afrika

KM Ban Ki-moon ametangaza taarifa maalumu iliyoyahimiza makundi yanayohasimiana Usomali kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kukomesha, halan, vitendo vyote vya umwagaji damu.”

WFP yarudisha tena huduma za kiutu Usomali kwenye maeneo ya mafuriko

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuanzishwa tena zile huduma za kupeleka misaada ya chakula kwenye maeneo ya Usomali yaliyoathirika na mafuriko, baada ya shughuli hizo kusimamishwa kwa muda pale mapigano yalipofumka katika wiki zilizopita.