Msaada wa Kibinadamu

Ndege zaanza kuingiza misaada Afghanistan

Ndege za shirika la Anga la Umoja wa Mataifa zinazosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP zimeanza tena safari zake za kupeleka msaada Kabul nchini Afghanistan na kuwawezesha wafanyakazi wa kibinadamu kuwafikia wananchi wenye uhitaji.

Tusipochukua hatua watoto milioni 1 wataangamia kwa unyafuzi Afghanistan:UNICEF

•     Watoto milioni 1 wako hatarini kwa utapiamlo
•    Zaidi ya milioni 9.5 wameacha shule wengi ni wasicha
•    Msaada unahitajika kunusuru afya yao na elimu

Msaada wa kisaikolojia watolewa kwa watoto nchini Afghanistan 

Nchini Afghanistan shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na washirika wengine wa maendeleo wanatoa huduma za msaada wa kisaikolojia kwa watoto zinazohusisha michezo na uchoraji bila kusahau utoaji wa chanjo kwa watoto chini ya miaka 5.

WFP yafanikisha ujenzi wa soko karibu na kambi ya wakimbizi nchini Msumbiji 

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwakushirikiana na wafanyabiashara wadogo, wamefanikiwa kujenga soko karibu na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Masquil Alto nchini Msumbiji na kupunguza adha ya wakimbizi kusafiri umbali mrefu kununua bidhaa.

Umoja wa Mataifa waendelea kuwasaidia watu wa Haiti kutokana na tetemeko la Agosti 14

Umoja wa Mataifa na wadau wake wa misaada ya kibinadamu wanaendelea kutoa misaada huko Les Cayes, Haiti baada ya tetemeko la ardhi lililoipiga kusini magharibi mwa nchi hiyo tarehe 14 mwezi uliopita likiharibu nyumba na miundombinu, kuua na kujeruhi maelfu ya watu.

Tunawahudumia kwa haraka Afar na Amhara lakini tunahitaji kuwezeshwa - WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limesema linashughulikia mara moja mahitaji yanayoongezeka na kuongeza msaada wa chakula cha dharura katika maeneo ya Afar na Amhara nchini Ethiopia. 

Visiwa vya Marshall vyajizatiti kupambana na janga la Corona 

Je unafahamu kuna nchi chache duniani ambazo mpaka sasa zimefanikiwa kujilinda na hazijapata hata mgonjwa mmoja wa Corona?. Moja ya nchi hizo ni Jamhuri ya visiwa vya Marshall. 

Mradi wa umwagiliaji wa sola wawanufaisha wakulima na kuokoa mazingira Bangladesh:FAO 

Nchini Bangladesh uhaba wa maji unatishia uzalishaji wa kilimo na maisha ya wakulima hasa kutokana na kutokuwa na mifumo bora ya uwagiliaji ambayo inasababisha upotevu wa maji. Lakini sasa changamoto hizo zinageuka historia baada ya shirika la chakula na kilimo FAO kuanzisha mradi wa mifumo bora ya umwagiliaji inayotumia nishati ya jua au sola kunusuru wakulima na mazingira.

Chakula cha msaada nchini Afghanistan kuisha mwanzoni mwa Oktoba:WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP nchini Afghanistan linatarajia kuishiwa akiba ya chakula mapema mwezi Oktoba mwaka huu na limeomba msaada wa fedha ili liweze kusaidia mamilioni ya watu kupata mlo.

Kilimo cha maharage kimeniinua kiuchumi na kuwalisha wanangu shuleni: mkulima Immaculée 

Kutana na mkulima Immaculée kutoka Rwanda ambaye anajivunia sio tu kupata kipato kujikimu kimaisha kutokana na mahindi na maharage anayolima bali pia jinsi mazao yake yanavyosaidia kuwa neema kwa mamia ya watoto kupitia mlo shuleni.