Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema mapigano kati ya jamii yaliyozuka katika eneo la Kaskazini nchini Cameroon katika wiki mbili zilizopita yamewafurusha takribani watu 100,000 kutoka katika makazi yao, ingawa idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi. Taarifa ya Jason Nyakundi inaeleza zaidi.