Msaada wa Kibinadamu

Chuo Kikuu cha wakimbizi kufunguliwa Kenya:UNHCR 

Umoja wa Mataifa unatambua kuwa wakimbizi nao licha ya kukimbilia ugenini kuokoa maisha yao, bado wana stadi mbalimbali na ujuzi ambao ukinolewa unaweza kuboresha siyo tu maisha yao bali pia maisha ya kule ambako wamesaka hifadhi.

Watoto zaidi watumikishwa jeshini Yemen

Kadri siku zinavyosonga hali ya kibinadamu nchini humo inazidi kuwa tete huku mapigano yakiendelea raia wakigharimika zaidi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejulishwa hii leo huku  likipatiwa mambo matatu ya kipaumbele ili kushughulikia janga hilo linaloelezwa kuwa ni kubwa zaidi la kibinadamu duniani.

Mlipuko wa kipindupindu wadhibitiwa miongoni mwa wakimbizi, Uganda

Licha ya idadi ya wakimbizi walioambukizwa maradhi ya kipindupindu nchini Uganda kuongezeka hadi 949 kutoka takribani wagonjwa 700 Ijumaa iliyopita, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, nchini humo limesema mlipuko huo umeanza kudhibitiwa.

Shughuli za kisiasa Burundi zimebinywa- Kafando

Nchini Burundi,  sintofahamu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyoanza baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kuongeza muda wa uongozi na kuingia awamu ya tatu bado inaendelea na sasa yaelezwa kuwa shughuli za vyama vya kisiasa zinaendeshwa na watu wachache.

Tunasaka misaada endelevu badala ya dharura pekee- UNHCR

Wakimbizi wanapowasili ugenini huduma ya kwanza ni mahitaji ya dharura kama vile maji, huduma  za afya na malazi kinachofuatia ni huduma za baadaye na endelevu. Mahitaji kama vile stadi za kazi na hata ajira.

Diplomasia ya kibinadamu “haiendi popote” nchini Syria.

Kwa miezi miwili sasa hakuna msafara wowote wenye misaada ya kibinadamu ambayo imewafikia raia walioko katika maeneo ya Syria yaliyozingirwa.

Dola bilioni 3 zahitajika kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na usaidizi wa kibinadamu na wakimbizi leo wametembelea kambi ya Kakuma nchini Kenya ili kushuhudia hali halisi ya kibinadamu wanayokabiliana nayo wakimbizi wa Sudan Kusini nchini humo. Taarifa zaidi na Patrick Newman.

Kuteketea makazi ya Kotobi ni msumari wa moto juu ya kidonda:UNMISS

Nchini Sudan Kusini baadhi ya jamii za waliotawanywa na machafuko wamejikuta hawana pa kulala baada ya makazi yao kusalia majivu yalipoteketezwa na moto. Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS watu hao awali walilazimika kuhama walikokuwa wakiishi kufuatia operesheni za kijeshi na sasa hawana pa kukimbilia. Siraj Kalyango na tarifa kamili