Msaada wa Kibinadamu

Raia wa Usomali 52 wakadiriwa kufariki kwenye Ghuba ya Aden, UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti wanakadiria raia wa Usomali 52 walifariki, [wiki iliopita] baada ya mashua iliotumiwa kuwavusha kimagendo kuelekea Yemen ilipoharibika na kuyoyoma kwa siku 18 bila ya chakula wala maji kwenye Ghuba ya Aden.

UNHCR imeripoti kupamba uhamiaji mkubwa wa raia Mogadishu

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kufanyika uhamiaji mkubwa wa raia waliong’olewa makazi kwa sababu ya mripuko wa mapigano yaliouvaa mji mkuu wa Usomali, Mogadishu katika siku za karibuni. Ron Redmond, msemaji wa UNHCR aliwapatia waandishi habari Geneva taarifa ziada juu ya tukio hilo kama ifuatavyo:~

Taathira mbaya kwa umma kufuatia mapigano Usomali zaitia wahka ICRC

Kadhalika Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) imetangaza kuwa na wasiwasi kuhusu taathira mbaya wapatazo umma kwa sababu ya mapigano yaliotanda Mogadishu karibuni. Msemaji wa ICRC, Anna Schaff aliwapatia waandishi habari Geneva Ijumaa tarifa ziada juu ya suala hili: ~~

WFP inaomba msaada wa kuhudumia chakula mamilioni Ethiopia

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza ilani maalumu ya maombi ya kufadhiliwa dola milioni 460 kuhudumia chakula watu milioni 9.6 katika Ethiopia ambao wameathirika vibaya sana kutokana na ukame uliotanda kwenye maeneo yao ikichanganyika na mifumko hatari ya bei za chakula.

Haki za Binadamu zinazorota Sudan, adai Sima Samar

Baraza la Haki za Binadamu Geneva leo limezingatia ripoti iliowasilishwa na Sima Samar, Mkariri Maalumu juu ya hali ya haki za binadamu katika Sudan. Alisema alipowasilisha ripoti, ya kwamba hali nchini humo bado inakabiliwa na vizingiti kadha wa kadha vyenye kutatanisha utekelezaji unaofaa wa haki za binadamu Sudan.

UNHCR imeripoti wahamiaji 26 kutoka Pembe ya Afrika wamezama Yemen

Mapema wiki hii Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti watu 120 waliokuwa wamesafirishwa kimagendo kutokea Pembe ya Afrika, na kuelekea Yemen, walilazimishwa, kwa kushikiwa bunduki, kuchupa kutoka mashua waliokuwemo katika Ghuba ya Aden, kitendo ambacho kilisababisha watu 26 kati ya umma huo kuzama na kufariki.

BU lashauriana juu ya hali katika JKK/msiba wa vimbunga Haiti

Wajumbe wa Baraza la Usalama Ijumaa asubuhi walishauriana, kwenye kikao cha faragha, kuhusu masuala yanayoambatana na hali katika JKK, na msiba wa vimbunga vilivyoathiri kihali Haiti na kuzingatia masuala mengine yanayohusu usalama na amani ya kimataifa.~

Mkuu wa UM anayesimamia misaada ya dharura anasihi fujo isistishwe Darfur

John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Mshauri wa KM kuhusu Misaada ya Dharura amenakiliwa akisema ana wasiwasi mkubwa juu ya ripoti alizopokea kuhusu kuendelea kwa fujo na vurugu katika Darfur. Alisema ripoti zimeonyesha karibuni kulifanyika mashambulio ya kijeshi katika Darfur Kaskazini na Jebel Marra, ikijumuisha mashambulio ya anga katika maeneo ya Birmaza na Disa na pia hujumu kadha dhidi ya wahudumia misaada ya kiutu zinazoendelezwa na makundi yenye kuchukua silaha.

UNICEF imeonya, watoto milioni 3 wa Pembe ya Afrika wanakabiliwa na utapiamlo hatari

Per Engebak, Mkurugenzi wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kwa ukanda wa Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki amenakiliwa akisema watoto karibu milioni 3 wanaoishi kwenye maeneo ya Pembe ya Afrika wanakabiliwa na hatari maututi ya utapiamlo mbaya na maradhi kadha wa kadha, kwa sababu ya kupungua kwa misaada inayofadhiliwa eneo hilo kutoka wahisani wa kimataifa.

Ndege ya kuhudumia misaada ya dharura katika JKK imeanguka

Ndege iliokodiwa na Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) kuhudumia misaada ya kiutu katika JKK iliripotiwa alasiri ya Ijumatatu ilijigonga na mlima, kilomita 15 kaskazini-mashariki ya Uwanja wa Ndege wa Bukavu wakati ilipokuwa ikielekea huko kutokea Kinshasa na ikichukua abiria 15 pamoja na marubani wawili, kwa mujibu wa taarifa za mwanzo tulizopokea kutoka msemaji wa OCHA Kinshasa, Christopher Illemassene.