Msaada wa Kibinadamu

Mvua kali na mafuriko yanahatarisha akiba ya chakula Afrika Magharibi: OCHA yahadharisha

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba nchi kadha za Afrika Magharibi zimeathirika na uharibifu unaochochewa na mfululizo wa mvua kali zilizonyesha huko katika siku za karibuni, hususan katika mataifa ya Burkina Faso, Mali na Togo.

Holmes kuzuru Myanmar kufuatilia huduma za kiutu

Mkuu wa UM anayehusika na misaada ya dharura, John Holmes amewasili Myanmar Ijumanne, kwa ziara ya siku tatu, kutathminia hali ya waathiriwa wa Kimbunga Nargis na maendeleo katika kufarajia misaada ya kiutu, pamoja na juhudi za Myanmar za kufufua tena huduma za kiuchumi na jamii. Baada ya kuwasili kwenye mji wa Yangon Holmes alipanda helikopta na kwenda moja kwa moja kwenye eneo la Delta la Ayeyarwardy, liliopo kusini, ambapo uharibifu mkubwa ulipofanyika mwezi Mei.mkulipotukia uharibifu mkubwa zaidi mwezi Mei kutokana na Kimbunga Nargis, tufani iliosababisha watu 138,000 ama kufariki au kupotea nchini. Shughuli za kufufua huduma za kiuchumi na jamii zinaendelea kukithiri, zikisimamiwa na mashirika kadha ya kimataifa yaliopo katika vituo sita vya Delta la Ayeyarwady. ~

WFP inaomba ulinzi wa manowari kwa meli zinazobeba chakula kwa Usomali

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakkula Duniani (WFP) imetangaza mjini London kuwa mashambulio yanayotukia Usomali dhidi ya wafanyakazai wa mashirika ya kimataifa yanayohudumia misaada ya kiutu ni mambo yanayohatarisha maisha ya mamilioni ya watu wenye kutegemea misaada ya chakula kutoka mashirika ya kimataifa.

UNHCR imepungukiwa fedha za kuhudumia wahamiaji wa Sudan Kusini

Jennifer Pagonis, Msemaji wa Geneva wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ameripoti kwa waandishi habari kuwa taasisi yao inakabiliwa na upungufu wa dola, karibu milioni 12, zinazotakiwa kushughulikia operesheni za kuwasaidia kihali wahamiaji wa Sudan Kusini waliodhamiria kurudi mwakao katika nusu ya pili ya mwaka. Huduma hizi zikikamilishwa zitawapatia wahamiaji hawo uwezo wa kuanzisha maisha mapya.

UM kutetea waathiriwa wa zilzala Uchina kupata misaada ziada ya kihali

Khalid Malik, Ofisa Mkaazi anayehusika na huduma za dharura Uchina, ametangaza kutokea mjini Beijing ya kwamba UM umeanzisha kampeni maalumu ya kuchangisha msaada wa dola milioni 33.5 wa kuwahudumia waathiriwa wa zilzala ya nguvu iliyotukia Mei 12 katika jimbo la Sichuan, tetemeko ambalo liliuwa watu 70,000 na kujeruhi mamia elfu wengine, na pia kusababisha zaidi ya watu milioni tano kukosa makazi.

Mzozo wa afya Ethiopia unakatisha tamaa, UM yaahidi kusaidia

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba tishio la kufumka kwa maradhi ya kuambukiza katika Ethiopia, ikichanganyika na tatizo la utapiamlo mbaya uliotanda kwenye maeneo kadha ni hali ambayo inakoroga huduma za kufadhilia mizozo ya kiutu yaiolivaa taifa hili la Pembe ya Afrika.~~ Sikiliza dokezo fafanuzi ya Paul Garwood, Msemaji wa WHO mjini Geneva kwenye idhaa ya mtandao.

Watalaamu wa UM/UU kuisaidia Philippines kudhibiti uharibifu wa sumu kutoka feri iliozama

Timu ya wataalamu wa UM na Umoja wa Ulaya (UU) hii leo wameelekea Philippines kuitika ombi la Serikali, ili kutathminia viwango vya sumu kali ya kemikali iliomwagika kutoka shehena ya mapipa ya dawa za kuua wadudu, yaliokuwa yamepakiwa kwenye ile feri iliozama karibu na Kisiwa cha Sibuyan, mnamo Juni 21 (2008), baada ya kupigwa na Kimbunga Fengshen.

Waathiriwa wa mafuriko Msumbiji wanahitaji suluhu ya kudumu, asema mtaalamu wa UM

Baada ya kukamilisha ziara ya uchunguzi nchini Msumbiji, Mjumbe wa KM juu ya Haki za Wahamiaji wa Ndani Waliong\'olewa Mastakimu, Walter Kaelin, alitoa mwito unaoitaka Serikali ya Msumbiji, pamoja na jamii ya kimataifa, kukuza juhudi za kuwapatia makazi na huduma nyengine za kuendeleza maisha ya kawaida wale watu walioharibiwa mali zao na mafuriko yaliojiri nchini humo miezi ya karibuni.

UM imewapatia watoto waathiriwa na utapiamlo Ethiopia chakula cha tiba

Mamia ya tani za Miranda Eeles, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo (UNICEF) ameripoti mbele ya waandishi habari Geneva, kama ifuatavyo, kwamba UM umetuma misaada ya chakula cha dharura Ethiopia kunusuru watoto waliokabiliwa na tatizo hatari la utapiamlo linalotokana na ukame:~~

Holmes ainasihi Zimbabwe kuondoa vikwazo dhidi ya wagawaji misaada

Mshauri wa UM juu ya Misaada ya Dharura, John Holmes, ameiomba Serikali ya Zimbabwe kuondosha vikwazo dhidi ya mashirika yasio ya kiserikali yaliopo nchini humo, kwa sababu vikwazo hivyo vinaathiri hali za watu milioni 2 nchini humo wanaotegemea misaada ya kimataifa kumudu maisha.