Msaada wa Kibinadamu

Zaidi ya watu laki 7 walioathiriwa na Kimbunga Gombe, Msumbiji bado wanahitaji usaidizi - IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) lina wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu ya watu zaidi ya 700,000 walioathirika katika Mkoa wa Nampula nchini Msumbiji, kufuatia kimbunga cha Gombe ngazi ya 3 ambacho kilianguka kwenye pwani kati ya wilaya za Mossuril na Mogincual tarehe 11 Machi.  

Watu milioni 18 Sahel kukabiliwa na njaa kali miezi mitatu ijayo:OCHA/CERF 

Watu wapatao milioni 18 kwenye Ukanda wa Sahel barani Afrika watakumbwa na njaa kali na kutokuwa na uhakika wa chakula katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu mwaka 2014 limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. 

Mradi wa Sola wa UNICEF watatua changamoto za waathirika wa ukame Kori Ethiopia 

Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF wa kuweka paneli za sola kwa ufadhili wa mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umeleta nuru kwa maelfu ya waathirika wa ukame katika eneo la Kori jimboni Afar nchini Ethiopia hasa tatizo la maji.

Mkutano wa kirafiki wakutanisha walinda amani kutoka Tanzania na baadhi ya viongozi mashariki mwa DRC

Kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na katika kuendeleza jukumu la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,  vikosi vya ulinzi wa amani kutoka Tanzania yaani TANZBATT 9 na kikosi cha utayari TANZANIA QRF2 vimefanya kikao cha Urafiki baina yao na uongozi wa raia wa nchi hiyo katika maeneo ya uwajibikaji wa vikosi hivyo.

Aliyoyashuhudia Martin Griffiths Kenya yamtisha, atoa wito wa haraka 

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Martin Griffiths, akihitimisha ziara ya siku mbili nchini Kenya ambapo alijionea athari mbaya ya msimu wa nne mfululizo wa mvua bila mvua katika Pembe ya Afrika. 

UNAIDS yashirikiana na wadau kuhakikisha wenye VVU nchini Ukraine wanapata huduma

Vita nchini Ukraine inaendelea kuathiri huduma katika sekta ya afya pamoja na minyororo ya ugavi ambayo mamia ya maelfu ya watu wanaoishi na ukimwi na walioathiriwa na virusi vya ukimwi, VVU wanategemea kuishi.

G7: FAO yatoa mapendekezo ya kukabiliana na uhaba wa chakula wa sasa na ujao

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO Qu Dongyu ametoa wito kwa nchi tajiri zaidi duniani G7 kusaidia kukabiliana na uhaba wa chakula katika siku zijazo kwani vita inayoendelea nchini Ukraine imepunguza usambazaji na kupandisha bei juu katika viwango vya kuvunja rekodi na kuyaweka mashakani mataifa ambayo tayari yana hatari ya kuathirika kote barani Afrika na Asia.

Ukame na vita vya Ukraine vimewaacha hoi wakulima nchini Somalia:IFAD

Mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD umeonya kwamba ukame na vita vinavyoendelea nchini Ukraine vimesababisha athari kubwa kwa wakulima nchini Somalia, ambao sasa wanahitaji msaada wa haraka ili kunusuru kilimo na maisha yao kabla hali haijageuka kuwa janga kubwa la kibinadamu. 

Hii si sahihi! Asema Mkuu wa OCHA baada ya kujionea hali halisi Turkana 

Ulimwengu umesahau madhila ya ukame wanayopitia watu wa Turkana, mvua haijanyesha Turkana.Tumeshuhudia misimu minne ya mvua zisizotabirika. Ni kauli ya Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Martin Griffiths baada ya kujionea hali halisi kwenye kaunti ya Turkana nchini Kenya hii leo. 

Wasyria milioni 26.5 wanahitaji msaada wa kibinadamu ndani na nje ya taifa lao:UN

Mgogoro wa Syria unaendelea kuwa changamoto kila uchao limesema shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA na kuongeza kuwa karibu watu milioni 26.5 wanahitaji msaada wa kibinamu ambapo milioni 14.6 wakiwa ndani ya Syria.