Msaada wa Kibinadamu

Juhudi za kidiplomasiya zachacha kusuluhisha mzozo wa Darfur

Tume ya Baraza la Haki za Kibinadamu iliyodhaminiwa madaraka ya kufanya uchunguzi kuhusu utekelezaji wa haki za kimsingi katika Darfur, majuzi ilichapicha ripoti yenye kuishinikiza Serekali ya Sudan kuharakisha uamuzi wa kuisaidia Umoja wa Mataifa (UM) pamoja na Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU)kupeleka vikosi vya mseto vitakavyotumiwa kulinda amani katika jimbo la Sudan magharibi la Darfur.

Maendeleo yaripotiwa Burundi kuhusu ulinzi wa watoto walioathirika na vita

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM kuhusu Hifadhi ya Watoto katika Mazingira ya Mapigano, alizuru Burundi wiki hii. Alisema kwamba ameshuhudia maendeleo ya kutia moyo katika juhudi za Serekali kuwapatia watoto walionaswa kwenye hali ya uhasama na vita, ulinzi bora na hifadhi inayotakikana kisheria.

Mashirika ya UM yahitajia dola milioni 18 kusaidia waathiriwa wa kimbunga na mafuriko Msumbiji

UM pamoja na mashirika wenzi yanayohudumia misaada ya kiutu, yameanzisha kampeni ya dharura kuchangisha karibu dola milioni 18 ili kuisaidia Msumbiji kukabiliana na mahitaji ya kihali, hususan kwa umma muathiriwa na mafuriko pamoja na uharibifu wa vimbunga, maafa ambayo yalisababisha uharibifu mkubwa nchini humo hivi karibuni.

Mahakama Kuu ya Zimbabwe kupongezwa na UM kwa uamuzi juu ya kiongozi wa upinzani

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour amenakiliwa akisema anaunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe ulioishurutisha Serekali kumruhusu kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC, Morgan Tsvangirai kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu baada ya kuthibitika kwamba alipigwa na kujeruhiwa vibaya na vikosi vya polisi alipokuwa kizuizini.

Hapa na pale

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limewaslisha wiki hii mjini Roma, Utaliana ripoti yenye mada isemayo "Hali ya Misitu Duniani 2007". Ripoti ilisema maeneo kadha duniani yamefanikiwa kudhibiti uharibifu wa misitu ulioendelezwa karne kwa karne. Kwa mujibu wa ripoti misitu kadha imefanikiwa kufufuliwa na kupanuliwa kwenye kanda mbalimbali za kimataifa kwa sababu ya usimamizi mzuri, na wa hadhari, ikichanganyika na sera za kisasa zilizotumiwa na mataifa husika katika kuhifadhi mazingira kwa ujumla. Ripioti ilisema mataifa 100 ziada hivi sasa yameandaa mipango ya kizalendo kuhifadhi misitu.

WFP inabashiria tatizo la njaa kusini ya Afrika

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuingiwa na wasiwasi unaoashiria kufumka, kwa mara nyengine tena katika maeneo ya kusini ya Afrika, janga la njaa kwa sababu ya kujiri karibuni kwa hali ya hewa ya kigeugeu. Hali hii imezusha ukame na mafuriko ambayo yaliharibu mavuno na kuathiri mamilioni ya watu watakaotegemea kusaidiwa chakula na jamii ya kimataifa kwa mwaka mzima.

UM unatarajia matokeo mazuri Usomali

Eric Laroche Mshauri wa UM kuhusu Misaada ya Kiutu kwa Usomali alipokutana na waandishi habari wa kimataifa hapa Makao Makuu wiki hii aliashiria ya kwamba Usomali, kwa sasa, imebahatika kushuhudia “vuguvugu la mabadiliko” yaliyowapatia umma matumaini ya kwamba Serekali mpya itajinyakulia fursa ya utawala iliyobarikiwa karibuni na kurudisha amani na utulivu katika taifa ambalo limenyimwa uongozi wa Serekali halali tangu 1991.~~

Msaada wa dharura unahitajika haraka CAR kunusuru maisha, yaonya UNICEF

Mia Farrow, msanii maarufu wa michezo ya kuigiza, ambaye pia ni Balozi Mfadhili wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) karibuni alizuru kwa siku nne sehemu za kaskazini za Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

WFP kununua chakula Msumbiji kuhudumia waathiriwa wa mafuriko

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa mwito wa kufadhiliwa, kidharura, msaada wa fedha zinazohitajika kununua chakula kutoka Msumbiji, taifa liliodhurika na mafuriko kusini ya Afrika. Lengo la hatua hii ni kunusuru maisha ya raia muhitaji 120,000 walioathiriwa na mafuriko yalizka hivi karibuni katika taifa hilo.

FAO imeitahadharisha Nigeria kuboresha udhibiti wa mifugo na kujikinga na H5N1

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limependekeza kwa Serekali ya Nigeria kuongeza huduma za kudhibiti afya katika masoko na mashamba ya kuku, kwa kuchanja mifugo ili kujikinga na hatari ya kutapakaa kwa virusi vya aina ya H5N1, ambavyo husababisha homa ya mafua ya ndege.