Msaada wa Kibinadamu

WFP imeanzisha tena ugawaji wa chakula Mogadishu

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) imeanzisha tena huduma za kugawa chakula, pamoja na huduma nyenginezo za kihali, kwa wakaazi na wahamaji 16,000 wa Mogadishu, Usomali mnamo wiki hii. WFP ilitarajiwa kuwapatia watu 114,000 msaada wa chakula mnamo mwisho wa wiki, ikijumuisha idadi ya wakazi waliohajiri mji baada ya vita kuanza, pamoja na wale ambao walishindwa kukimbia mapigano na kunaswa ndani ya mastakimu yao wakati uhasama uliposhtadi.

Msaada mpya kwa WFP kuashiria mwisho wa mgawo wa dharura Uganda

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) imepokea msaada wa yuro milioni 5 kutoka Ofisi ya Misaada ya Kiutu ya Kamisheni ya Ulaya (ECHO) pamoja na mchango ziada mwengineo ambao tuliarifiwa utatumiwa kugawa chakula kwa watu milioni 1.28 waliong\'olewa makwao nchini Uganda. Msaada huu utaipatia WFP fursa ya kurudisha posho kamili ya chakula kwa umma huo muhitaji ambao siku za nyuma walialzimika kupatiwa posho haba kwa sababu ya upungufu wa misaada ya kuendeleza shughuli hizo.

UNICEF yasaidia watoto 60,000 kupata vifaa vya maskuli

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetuma misaada ya vifaa vya skuli kwa wanafunzi watoto 60,000 waliopo kwenye yale maeneo sita ya Zambia yalioathiriwa na mafuriko yaliogharikisha sehemu hizo za nchi hivi karibuni.

Hapa na pale

Waundaji sera za kitaifa pamoja na wataalmu kutoka ulimwengu wa taaluma, sayansi na biashara wamekutana mjini Trieste, Utaliana kwenye mkutano wa siku tatu, ulioandaliwa na mataifa ya G-8 pamoja na UNESCO, kuzingatia hatua za kuchukuliwa kimataifa kuhamasisha maendeleo ya kudumu, kwa kutumia mfumo wa kufungamanisha matumizi ya uvumbuzi wa teknolojia ya kisasa, utafiti wa kisayansi na ilimu.

--FAO kupendekeza marekibisho ya ugawaji wa chakula katika nchi zinazoendelea--Utekelezaji wa haki za binadamu katika Darfur

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) hivi karibuni liliwasilisha ripoti ya mwaka ambayo ilifanya mapitio juu ya Hali ya Chakula na Kilimo Duniani, ripoti ambayo hujulikana kwa umaarufu kama Ripoti ya SOFA. Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jacques Diouf alipoiwakilisha kwa mara ya kwanza ripoti hiyo alikumbusha ya kwamba wakati umewadia, kwa wahisani wa kimataifa kurekibisha huduma za ugawaji wa misaada ya chakula duniani.

Sudan kupatiwa msaada wa ngano wa dola miloni mbili kutoka Urusi: imeripoti WFP

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), limepokea kutoka Urusi, msaada wa ngano, wa dola milioni 2, uliokusudiwa kufufua tena zile operesheni za kuwapatia chakula watoto wa skuli muhitaji karibu 300,000 waliopo kwenye majimbo matatu ya Sudan yaliokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.

WFP imeanzisha operesheni za kuhudumia waathiriwa wa kimbunga Bukini

Shirika la WFP limeanzisha misafara ya ndege, za kupeleka chakula na misaada ya dharura inayohitajika kuwahudumia kihali maelfu ya watu wanaoishi kaskazini-magharibi ya Bukini, eneo ambalo hivi karibuni lilichafuliwa vibaya na kimbunga kilichoharibu vibaya sana barabara na madaraja.

KM kulitaka Baraza la Usalama (BU) kuanzisha mazungumzo ya amani kwa Sahara ya Magharibi

Ripoti ya karibuni ya KM juu ya Sahara ya Magharibi imependekeza kwa Baraza la Usalama kuwaita Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi cha Frente Polisario, kushiriki, bila ya shuruti, kwenye mazungumzo ya kuleta suluhu ya kuridhisha, na ya kudumu, itakayoupatia umma wa Sahara ya Magharibi fursa ya kujichagulia serekali halali ya kuwawakilisha kitaifa.

Matatizo ya kiutu kukithiri katika CAR

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba hali mbaya ya kiutu inaendelea kusambaa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ambapo mamia elfu ya raia waliong’olewa makwao, kwa sababu ya hali ya vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, wanahitajia kufadhiliwa kidharura misaada ya chakula kunusuru maisha. Hali hii sasa hivi imechafuliwa zaidi kutokana na vurugu liliofumka na kufurika kutokea eneo jirani la Darfur, Sudan.

Mapigano makali Usomali kuzusha msiba mkuu wa kiutu nchini: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba hali ya kijamii, kwa ujumla, katika Usomali, ni mbaya sana kwa sasa, kutokana na mapigano makali yalioshtadi karibuni, vurugu ambalo aina yake haijawahi kushuhudiwa tangu 1991.