Msaada wa Kibinadamu

Madaraja yanayojengwa na MINUSCA CAR yaleta imani kwa wananchi

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, madaraja yaliyojengwa kwa ufadhili wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSCA, yamesaidia kuimarisha doria zinazofanywa na walinda amani wakiwemo wale wanaotoka Tanzania na hivyo kuimarisha usalama na kurejesha matumaini kwa wakazi wa maeneo ya Gamboula na Noufou. Jason Nyakundi na ripoti kamili

Fistula yaendelea kuwa jinamizi kwa wanawake wakati wa kujifungua:UNFPA

Licha ya tahadhari na jitihada kubwa zinazofanyika kote duniani kuwanusuru, ugonjwa wa Fistula umeendelea kuwa ni jinamizi linalowaghubika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA. 

Pamoja na ukarimu wake sasa Afrika yalemewa na mzigo wa wakimbizi:UN

Afrika imepongezwa kwa ukarimu wake hasa wa kupokea mamilioni ya watu wanaosaka usalama wakikimbia vita na utesaji. Hata hivyo  idadi ya watu wanaotawanywa na kulazimika kukimbia makwao hadi kufikia mwisho kwa mwaka 2017 ilikuwa milioni 24.2 , na kulibebesha mzigo mkubwa wa kiuchumi bara hilo. 

WFP yafikiria kusitisha utoaji misaada sehemu zinazodhibitiwa na Houthi nchini Yemen

Shirika la mpango wa chakula dunia WFP linataka mambo matatu ya dharura kufanyika nchini Yemen yakiwemo: uhuru wa kuhudumu, kuwafikia wale walio na njaa na kufanyika usajili wa kieletroniki.

Hakuna uhalali wowote wa kuwashambulia raia Afghanstan-UNAMA

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa nchini Afghanistan, ameeleza kusikitishwa kwake na ongezeko la vurugu katika maeneo mbalimbalimbali ya nchi wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Wakimbizi wa Syria waanza kujirejesha nyumbani taratibu

Nchini Syria baadhi ya wananchi waliokimbia makazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka nane sasa, wameanza kurejea kwenye mapagala yao ingawa kazi ya  ujenzi mpya inasalia kuwa na changamoto kubwa.

Nuru ya amani yamulika mji wa Kapoeta nchini Sudan Kusini

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa umekuwepo kwenye mji wa Kapotea jimbo la Namorunyang  nchini Sudan Kusini kwa lengo la kuimarisha ujenzi wa amani na hatimaye wakazi wake waliokimbia kutokana na mapigano waweze kurejea.
 

WHO yalaani shambulizi la gari la wagonjwa Tripoli

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limelaani vikali shambulio dhidi ya gari la wagonjwa kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli ambalo limejeruhi wahudumu watatu wa afya, mmoja wao hali yake ikiwa mbaya zaidi.

Ulinzi wa haki ya mtoto ni msingi wa mafanikio ya mkataba wa amani CAR- Gamba

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye mizozo, Virginia Gamba amehitimisha ziara  yake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR akisema usaidizi madhubuti kwa wavulana na wasichana walioathirika na mzozo nchini humo ni jawabu mujarabu la kufanikisha mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Februari mwaka huu. 

WHO yaja na mpango mpya wa chanjo dhidi ya Ebola.

Jopo la ushauri wa kimkakati kwa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu masuala ya chanjo, SAGE, limetoa mapendekezo mapya katika kushughulikia changamoto wanazokumbana nazo katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.