Msaada wa Kibinadamu

WFP kupunguza mgao wa chakula kwa wayemen kuanzia  mwezi ujao, kisa? Ukata!

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP hii leo limeonya kuwa linaendelea kukumbwa na uhaba wa fedha za kuendesha operesheni zake za  kusambaza msaada wa chakula kwa watu milioni 13 nchini Yemen na kwa hiyo litalazimika kupunguza mgao wa chakula kwa baadhi ya wananchi kuanzia mwezi ujao wa Januari.

Dola bilioni 1.5 zahitajika kunusuru Somalia mwaka 2022

Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu nchini Somalia hii leo wametangaza mpango wa usaidizi wa kibinadamu nchini humo kwa mwaka 2022 mpango ambao unahitaji jumla ya dola bilioni 1.5 kwa ajili ya kusaidia watu milioni 5.5 wanaokabiliwa na hali ngumu ya kibinadamu.

Katibu Mkuu wa UN afanya ziara nchini Lebanon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka viongozi wa Lebanon kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua migogoro iliyopo nchini humo, huku akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha kuiunga mkono Lebanon kutokana na matatizo yake ya sasa.

Kimbunga Rai au Odette chasababisha madhara Ufilipino, mashirika ya misaada yanajipanga

Baada ya kutua kwa mara ya kwanza huko Siargao, Surigao del Norte jana tarehe 16 Desemba, Kimbunga Rai (kinachoitwa Odette nchini humo), leo Desemba 17 kimepitia katika baadhi ya maeneo ya kusinimagharibi mwa Ufilipino kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 155 kwa saa, na karibia  upepo mkali wa hadi kilomita 235 kwa saa katika kitovu chake.  

HRC kuanzisha tume ya kimataifa kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu Ethiopia

Wasiwasi mkubwa wa madai ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili mwingine nchini Ethiopia unapaswa kuchunguzwa na chombo cha kimataifa cha haki za binadamu, limeafiki Baraza la Haki za Kibinadamu hii leo kupitia kura maalum. 

Mlipuko wa karibuni wa Ebola wakunja jamvi DRC: WHO

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limetangaza kwamba mlipuko wa Ebola uliozuka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini mwezi Oktoba ukiwa ni wa pili kwa mwaka 2021 sasa umemalizika. 

Visa vipya vya COVID-19 vyapungua duniani: WHO

Ripoti mpya ilitolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kuhusu janga la COVDI-19 inaonesha matukio ya kila wiki ya visa vipya vya wagonjwa yamepungua kwa asilimia 5 na vifo vinavyohusiana na janga hilo vikipungua kwa asilimia 10 katika wiki ya kuanzia tarehe 6 mpaka 10 Desemba 2021.

UN yaanza utoaji chanjo kwa wahamiaji 7,500 waliokwama Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM leo limeanza kampeni ya chanjo ya COVID-19 kwa wahamiaji waliokwama nchini Yemen.  

Joyce Msuya kuwa msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu na kaimu wa OCHA

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo metangaza kumteua Bi Joyce Msuya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa msaidizi wa wa Katibu Mkuu kwa masuala ya kibinadamu na naibu mratibu wa misaada ya dharura katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA. 

UNFPA yahitaji dola milioni 835 kusaidia wanawake na wasichana katika nchi 61 mwaka 2022

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu na afya ya uzazi duniani UNFPA, hii leo limezindua ombi maalum la dola milioni 835 likiwa ni ombi lake kubwa zaidi la kibinadamu ili liweze kuwafikia zaidi ya wanawake, wasichana na vijana milioni 54 katika nchi 61 mwakani 2022 kwa ajili ya kutoa msaada muhimu.