Msaada wa Kibinadamu

Wanaotegemea msaada wa kibinadamu wana hali tete

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo FAO na la mpango wa Chakula duniani WFP yameeleza jitihada za kupambana na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama wa chakula zinazofanyika katika nchi kadhaa zinashindikana kutokana na kuwepo kwa mapigano na vizuizi ambavyo vimekwamisha ufikishaji misaada ya kuokoa maisha ya familia zinazokabiliwa na njaa. 

Ziara yetu Tigray imethibitisha hali tete inayokabili watoto- UNICEF

Hali tete iliyokuwa inadhaniwa kukumba watoto jimboni Tigray nchini Ethiopia sasa imethibitishwa baada ya watendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuweza kufika eneo hilo baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa miezi kadha kutokana na ukosefu wa usalama.
 

Ndege ya Umoja wa Mataifa yapata ajali nchini Ethiopia

Ndege ya ofisi ya Umoja wa Mataifa la utoaji wa huduma za kibinadamu, (UNHAS) inayosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani -WFP imepata ajali  jana tarehe 27 mwezi huu wa Julai huko nchini Ethiopia wakati ikisafirisha watoa huduma kutoka Jigjiga kwenda Dire Dawa.

UNHCR yawajengea nyumba wakimbizi wa ndani DRC

Machafuko yanaendelea Jimbo la Kivu kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia Kongo, DRC yanasababisha kila uchwao wananchi wa eneo hilo kuyakimbia makazi yao kwenda kuishi mikoa ya jirani.

Marekani kutoa milioni 135.8 kusaidia wakimbizi wa kipalestina

Shirika la Umoja wa Mataifa la usaidizi kwa wakimbizi wa kipalestina - UNRWA limetangaza Marekani inachangia milioni 135.8 ilikuwezesha kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wakimbizi. 

Ziwa Tanganyika laendelea kufurika, Burundi wahaha, IOM na wadau waingilia kati

'Tutafanya nini iwapo maji yataendelea kujaa?’ Hilo ni swali lililogubika kila mtu: Wamiliki wa nyumba, wakandarasi wa ujenzi, wajenzi, wakulima, wachuuzi sokoni, wanafunzi, wasafiri na bila shaka wafanyakazi wa maendeleo na kibinadamu.
 

Msaada wa fedha kwa wakimbizi wazidisha amani baina ya wakimbizi na wenyeji Uganda 

Uganda nchi inayoongoza kuhifadhi wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, imeshuhudia kuongezeka kwa mahusiano mema baina ya wakimbizi na wananchi waliowakaribisha baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP, kuanza kutoa msaada wa kifedha kwa wakimbizi hali inayowawezesha wakimbizi kununua bidhaa kutoka kwa wanajamii pamoja na wao wenyewe kufungua biashara zao.

Hatimaye shehena za misaada ya kibinadamu zaingia Tigray- WFP

Msafara wa malori 50 ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP yaliyosheheni misaada ya kibinadamu leo hii hatimaye yameingia Mekelle mji mkuu wa jimbo la Tigray nchini Ethiopia baada ya vuta ni kuvute ya muda mrefu.

Walipiga watu risasi na kuwakata vichwa- Simulizi ya machungu kutoka Cabo Delgado 

Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji limekumbwa na ghasia tangu mwaka 2017. Eneo hilo lipo mpakani mwa Tanzania na limeshuhudia ghasia hizo zikifurusha wengine kuvuka mpaka  kuingia Tanzania na wengine kukimbilia maeneo mengine kusaka hifadhi ndani ya nchi yao. Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake likiwemo lile la mpango wa chakula, unahaha kukidhi mahitaji ya kibinadamu. Lakini hali iko vipi kwa wananchi hao? Na Umoja wa Mataifa unataka nini kifanyike zaidi?

Idhini ya kuvusha misaada ikikoma Julai 10, Wasyria watakuwa hatarini zaidi - OCHA 

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya kibinadamu, OCHA, imeonesha wasiwasi wake kuwa ifikapo tarehe 10 mwezi huu wa Julai,  kushindwa kuongeza idhini iliyowekwa na Baraza la Usalama la UN ya kuvusha misaada ya kibinadamu kutaongeza viwango vya mateso kwa raia ambavyo ambavyo havijaonekana katika kipindi cha miaka 10 ya mgogoro wa Syria.