Kupitia katika ujumbe wa video kwa Mkutano wa tano unaofanyika Brussels, Ubelgiji, kuunga mkono Syria na ukanda huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa wafadhili kusaidia kushughulikia mahitaji yanayoongezeka na kuongeza ahadi za kifedha na kibinadamu kuwasaidia Wasyria na "kupunguza mzigo mkubwa wa kifedha wa nchi ambazo zinahifadhi wakimbizi.”