Msaada wa Kibinadamu

Walinda a.mani wa Umoja wa Mataifa wachangia damu Lebanon

Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake na wadau, wameendelea kutoa misaada kwa waathirika wa mlipuko uliotokea Agosti 4 katika mji mkuu wa Lebanon Beirut. Takribani walinda amani 100, wanajeshi na raia, wamejitolea kuchangia damu kwani bado uhitaji ni mkubwa. 

Tunasema asante kwa wahudumu wa kibinadamu kokote waliko katika kuokoa maisha-OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibindamu na masula ya dharura OCHA, imeeleza kuwa janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 limeongeza machungu katika changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo watoa huduma za kibinadamu kote duniani

Wahudumu wa kibinadamu ni mashujaa wanaoweka rehani maisha yao ili kuokoa ya wengine:Guterres

Ikiwa leo ni siku ya huduma za kibinadamu duniani Umoja wa Mataifa umesema unawaenzi wahudumu hao ambao wanakabiliana na changamoto lukuki katika kuokoa na kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. 

Watoto Haiti na uelewa wa kina jinsi ya kujikinga na COVID-19

Kampeni iliyoendeshwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na Wizara ya Afya ya Umma na Idadi ya watu nchini Haiti kuhusu jinsi ya kujikinga na virusi vya Corona, au COVID-19, imekuwa na mafanikio katika kupunguza maambukizi na hata watoto wana uelewa.

WFP kupeleka unga wa ngano na nafaka nchini Lebanon

Ili kusaidia kupambana na uhaba wa chakula nchini Lebanon baada ya mlipuko uliotokea tarehe 4 Agosti mwaka huu, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, linapeleka nchini humo unga wa ngano na nafaka katika kipindi hiki ambacho nchi inajenga upya bandari yake na imesaliwa na hifadhi ya unga wa ngano inayokadiriwa kukidhi mahitaji ya soko kwa kipindi cha wiki sita.

UN4Beirut na mshikamano na wananchi wa Lebanon

Nchini Lebanon, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wamezindua kampeni iitwayo Umoja wa Matafa kwa ajili ya Beirut, au UN4Beirut kwa lengo la kuonesha mshikamano na kusaidia watu wa Lebanon kusafisha mitaa ya mji huo mkuu uliosambaratishwa na mlipuko mkubwa wa tarehe 4 mwezi huu wa Agosti. 

UNICEF yatoa msaada kwa watu 40,000 waliotawanywa na machafuko mapya Kivu Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linatoa msaada muhimu wa kibinadamu kwa watu 40,000 ambao wamekimbia machafuko ya kikabila katika eneo la milimani la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Waliokufa katika mlipuko Beirut ni pamoja na wakimbizi 34: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limesema limeshtushwa na taarifa kwamba miongoni mwa watu zaidi ya 200 waliopoteza misha kwenye mlipuko mkubwa wa Beirut uliotokea Agosti 4 nchini Lebanon wanajumuisha angalau wakimbizi 34 hadi sasa. 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaendelea na juhudi za kuokoa maisha Beirut

Ikiwa leo ni siku ya saba tangu kutokea mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umeendelea kufanya kila juhudi za kuokoa maisha na kurejesha hali ya kawaida katika mji huo ambao ni kiini cha maisha ya nchi hiyo iliyoko  mashariki ya kati.

Misaada yaelekezwa Beirut, OHCHR yataka uchunguzi wa kina

 Siku tatu tangu mlipuko mkubwa kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa kwenye mji mkuu wa Lebanon, Beirut, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake wanapeleka misaada ya hali na mali huku ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikitaka uchunguzi wa kina na mamlaka ya thabiti ili kuepusha hali kama hiyo isitokee tena.